DK.Kigwangalla akutana na wafanyakazi MOI, aunda kikosi kazi kushughulikia kero zao na taasisi

507
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema asubuhi ya leo Machi 22.2017, amekutana na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kufanya nao mazungumzo ikiwemo kupokea maoni na kero zao mbalimbali ambapo alizipokea huku akiunda kikosi kazi maalum cha kushughulikia kero hizo.

Awali Dk. Kigwangalla aliweza kupokea kero hizo kutoka kwa wafanyakazi na baadae Madaktari na watendaji wa taasisi hiyo, hata Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali ina nia njema na inaimipango mizuri ikiwemo kusaidia Idara na Taasisi zake hususani za sekta ya Afya kiasi cha kuongeza bajeti kubwa kwenye upande huo.

“Nimekuja hapa kujifunza na na kupata uzoefu pamoja na kuwasikiliza. Toka nimeteuliwa sikuwahi kuja hapa katika tukio kama hili. Muhimbili nilishafika ila kwa leo kuja kuwasikiliza naamini Serikali yetu ni sikivu. Changamoto za vifaa tiba nimeisikia na matatizo yote nayachukua kwenda kuyafanyia kazi” amesema Dk. Kigwangalla.

Akizungumzia juu ya mradi wa awamu ya tatu ya jengo la MOI ambalo anaamini litaondoa kero kwa asilimia kubwa inayoikumba Taasisi hiyo, ameamua kuunda kikosi kazi maalum ili kushughulikia na mradi huo ukamilike.

“Mradi huu wa awamu ya tatu wa jengo la MOI, zaidi ya asilimia 50 ya matatizo yanayoikabili MOI yatamalizika pindi utakapokamilika.

Mradi wa maboresho wa vyumba vya upasuaji vyetu hapa MOI vinashughulikiwa na maboresho hayo yatasaidia kurudisha ubora wake kama hapo zamani. Nawathibitishia kwamba, kwa sasa nitashughulikia mambo haya na nitasimamia kwa ukaribu sana na kuhakikisha mradi huu wa awamu ya tatu wa MOI unakamilika na utaondoa msongamano mkubwa wa wagonjwa, vifaa vibovu ambavyo nikipita naviona huko kwenye makolido” alimalizia Dk. Kigwangalla.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, vymba vya upasuaji (Theater) katika taasisi hiyo ya MOI vilikuwa vya viwango vya juu kwa miaka 15 iliyopita hivyo anaamini suala hilo kwa sasa atalisimamia kwa nguvu zote mpaka kukamilisha hasa mradi huo wa awamu ya tatu.

Katika kufikia malengo hayo, Dk. Kigwangalla ameweza kuunda kikosi kazi maalum cha kuiboresha taasisi ya MOI ambapo kitaongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasiyo yakuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Profesa Ayubu Magimba huku katibu wake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma na watasaidiwa na wajumbe wengine wakiwemo Madaktari bingwa waliofanya kazi kwa muda mrefu katika taasisi hiyo.

Dk. Amekiagiza kikosi hicho kuhakikisha kinashughulikia kuondoa kero juu ya upatikanaji wa vifaa ikiwemo suala la vifaa tiba hasa vile  vifaa pandikizi (Implant), Namna ya kutengeneza makambi ya upasuaji siku za wiki ili kupunguza msongamano wa wanaosubiri kufanyiwa operesheni (upasuaji), Kufuatilia dhamana ya Serikali baina ya Taasisi hiyo na Wizara ya Afya juu ya kupata fedha upya za kumalizia mradi huo wa awamu ya tatu ya jengo la MOI.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dkt. Othman Kiloloma amesema kuwa mbali na changamoto wanazokabiliana nazo, wameweza kuwa na mipango mbalimbali ikiwemo kuwa na kambi maalum za upasuaji ambazo zinafanyika siku za wiki  kwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa kwa siku za Jumamosi na  Jumapili kwani zoezi hilo ni moja ya njia ya kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaosubiria huduma hiyo.

Kwa upande wao Madaktari na wafanyakazi wa MOI wamepongeza ujio huo wa Naibu Waziri kwani wameweza kutoa kero zao na kupatiwa majibu ya kina huku majibu ya kero zao mengine yakitarajiwa kupatiwa ufumbuzi hapo baadae kama alivyowaahidi.

Picha ya mchoro wa mradi huo wa awamu ya tatu ya jengo la MOI.

Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dkt. Othman Kiloloma akitoa taarifa za taasisi hiyo ya MOI wakati wa tukio hilo la Naibu Waziri Dkt. Kigwangalla (kulia) alipotembelea mapema leo Machii 22.2017

Sehemu ya wafanyakazi wa MOI wakifuatilia tukio hilo

Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dkt. Othman Kiloloma akimkaribisha Dk. Kigwangalla kusema wakati wa tuko hilo la kuongea na wafanyakazi wa taasisi hiyo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akuzungumza na wafanyakazi  wa MOI (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo mapema leo Machi 22.2017.

Baadhi ya wafanyakazi wa MOI wakifuatilia tukio hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea swali  kutoka kwa wafanyakazi wa MOI ambao walikuwa wakiuliza na kuwajibu

Wafanyakazi wa wakiuliza maswali kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla

Wafanyakazi wa wakiuliza maswali kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla

Wafanyakazi wa wakiuliza maswali kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla

Wafanyakazi wakifuatilia tukio hilo

 Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akizungumza na wafanyakazi hao

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akiwa amemsimamisha Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Kiloloma (kushoto) kujibu baadhi ya maswali ya taasisi hiyo

 Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akifafanua namna  Serikali ilivyojipanga kusaidia taasisi hiyo ya MOI

 Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akipitia baadhi ya nyaraka wakati wa tukio hilo

aibu Waziri Dk. Kigwangalla akisindikizwa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk.Kiloloma.

MO BLOG

Share:

Leave a reply