Dk.Kigwangalla: “RC Amos Makalla shujaa wa Mapinduzi ya Afya ya Msingi (PHC)

326
0
Share:

Anaandika, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla:

Kwenye mfumo wa Afya Tanzania, Rufaa huanzia ngazi ya kaya/jamii, kwenda kwenye Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya Wilaya, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Hospitali Maalum/Taifa mpaka nje ya nchi. Hakuna nchi hapa Africa Mashariki inayowajali wananchi wake kiasi cha kuwapa fursa pana ya Rufaa zaidi ya sisi.

Ni Tanzania pekee. Wengine wanabeza kuwa kwa nini tusitibiwe hapa hapa tu mpaka twende nje ya nchi? Kwetu sisi hii ni kutanua fursa ya wanna go kupata ‘second opinion’ kwa wenzetu na pia kupata fursa ya matibabu kwenye magonjwa ambayo hatuna utaalamu nayo. Lengo letu ni kujenga uwezo wa ndani kwa kasi ili tufikie kuwa na wagonjwa wachache sana wenye kupelekwa nje ya nchi.

Katika mnyororo huu wa rufaa, kwa mtazamo wangu, mahala pa muhimu zaidi ni kule chini kabisa: kuanzia kwenye jamii mpaka kwenye ngazi ya Hospitali ya Wilaya. Huku kuna wananchi wengi wanaohudumiwa na huu ndiyo msingi wa kutoa fursa sawa kwa watu wote. Ndiyo maana kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM tulisema tutajenga Zahanati kwenye kila kijiji na tutajenga Kituo cha Afya (Health Center) kwenye kila Kata. This is indeed a tall order, an ambitious goal!

Tumeanza kutekeleza agizo hili la ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kujenga Vituo Vipya vya Afya 100, na kukarabati vilivyopo 489 ili viweze kukamilika na kutoa huduma za Maabara na za upasuaji kama Sera ya Afya inavyoelekeza. Kabla ya hapa, kati ya vituo takriban 489 vilivyokuwepo, ni 113 tu vilikuwa na huduma ya upasuaji.

Rafiki yangu na Kaka yangu, Ndg. Amos Gabriel Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza, Shujaa wa Afya, na ataacha alama ya milele kwenye Mkoa wake, kwa kuwa anaongoza mapinduzi makubwa ya ujenzi wa Vituo vya Afya kila Kata na ujenzi wa Zahanati kila Kijiji.

Amewaunganisha Wataalamu, viongozi wa Mkoa na Wilaya wa serikali, wa dini, wa Mila na wananchi wote nyuma ya hii ndoto yake! Ameagiza na anafuatilia kuhakikisha kabla ya juni 2017 wananchi wawe wamekamilisha maboma na Halmashauri ziwe zimeweka bajeti ya kuyamalizia.

Ameifanya hii ndiyo agenda yake ya kipaumbele na ya kudumu. Anasema hii ni alama yake. Mungu amuongoze.
Ndg. Makalla, nakuhakikishia ukikamilisha hili, utatukuzwa leo duniani na Mungu atakupa pepo na mwangaza wa milele kesho akhera! Huu ndiyo uongozi wenye kuacha alama!

Mkakati huu unawalenga wananchi wa chini. Sauti ya hawa ni sauti ya Mungu. Ndg. Makalla atakuwa Mkuu wa Mkoa wa mfano kusimamia hili! Na sisi tutamuunga mkono.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Regional Commissioner-RC), Mh. Amos Makalla.  

 

Share:

Leave a reply