Dk.Mwakyembe apongeza Vietnam kwa kuimarisha mahusiano ya Kidiplomasia na Uchumi na Tanzania

263
0
Share:

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amempongeza Balozi Vo Than Nam wa Vietnam anayemaliza kipindi chake nchini, kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Vietnam na Tanzania kwa kiwango cha juu.

Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 71 ya uhuru wa Vietnam kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana jioni iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya mabalozi nchini, Waziri huyo alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya Vietnam ya Halotel katika sekta ya mawasiliano ni moja ya mafanikio makubwa ya mahusiano ya nchi zetu mbili.

Ambapo ameweka wazi kuwa, milango iko wazi kwa makampuni zaidi kutoka Vietnam kuwekeza chini katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa uzoefu ambao Vietnam imeupata katika mageuzi yake ya uchumi kutoka uchumi wa kilimo hadi wa viwanda ni chachu kwa Tanzania inayofuata njia hiyohiyo.

Akimkaribisha Waziri huyo aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo, Balozi Vo Than Nam aliwasifu Watanzania kwa moyo wa ushirikiano na kuahidi kuendeleza mahusiano kati ya nchi zote mbili.

mwakyembeBalozi Vo Than Nam wa Vietnam anayemaliza kipindi chake nchini, akizungumza machache wakati wa tukio hilo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe

vietnamWaziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia tukio hilo. kulia kwake ni Balozi Vo Than Nam wa Vietnam anayemaliza kipindi chake nchini.

Share:

Leave a reply