Dk. Nchemba awahakikishia wananchi usalama

166
0
Share:

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba amewahakikishia usalama wananchi wote ambao majimbo yao yanafanya uchaguzi wa marudio na kuwataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura pasipo kuhofia usalama wao.

Dk. Nchemba amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayeshiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani katika uchaguzi huo.

Akizungumza katika kampeni ya kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini ndugu Monko, Dk Mwigulu aliwataka wananchi kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kumchagua Monko ili awaletee maendekeo kwani kiongozi wakiomchagua awali ameonekana kushindwa kuendana na kazi ya Rais Dk Magufuli.

“CCM ina watoto wengi mmoja akisema amechoka baada ya kutumwa sana unamchukua mwingine na kumtuma, Monko anauwezo mkubwa wa kuwasaidia kuwaletea barabara na umeme ambao mmeukosa mpeni yeye atawasaidia,” alisema Waziri Mwigulu 

Naye mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Justine Monko amewataka wananchi kumpigia kura nyingi ili aweze kuwaletea maendeleo kwa kuwajengea zahanati, barabara, na umeme ambao wameukosa kwa mda mrefu kwani anauzoefu na ameshawai kuwa mkurugenzi wa halmashauri.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Singida, Juma Kilimba amesema wanauhakika wa kushinda kwa asilimia kubwa kwani wamefanya kampeni kwa kata zote 21 na wananchi wanaimani kubwa na mgombea na Chama cha Mapinduzi.​

Share:

Leave a reply