Dk.Tulia Akson: “Watanzania tuuenzi Utamaduni wetu”

495
0
Share:

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Tulia Ackson (Mb.) amewaasa Watanzania kuuenzi  Utamaduni kupitia Sanaa.

Akizungumza katika uzinduzi maalum wa mafunzo ya Sanaa kwa vijana 27 kutoka Mkoani Mbeya,  Dk. Tulia kupitia taasisi yake ya Tulia Trust amesema kuwa, kupitia taasisi hiyo imeamua kuuenzi utamaduni wa Mtanzania kupitia vijana hao ambao watapata mafunzo ya Sanaa na Utamaduni ili kuwa mabalozi wazuri kwenye  tasnia ya Sanaa na Utamaduni hapa nchini.

Dk.Tulia ameeleza kuwa, Vijana hao 27 kutoka Wilaya za Rungwe, Busokelo na Kyela, Mkoa wa Mbeya wamepata ufadhili huo kutokana na umahiri wao waliouonesha katika shughuli za tamasha linaloandaliwa na taasisi hiyo huko Mkoani Mbeya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni  Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye  vijana hao wagharamiwa mafunzo  ikiwemo pamoja  na kulipia ada za masomo, chakula, malazi na usafiri kwa muda wote wawapo Chuoni hapo.

Wanafunzi hao tayari wapo Chuoni hapo wakiendelea na mafunzo hayo ya Sanaa na Utamaduni yanayotolewa na wakufunzi mabingwa na mahiri wa taasisi hiyo ya Sanaa ambayo ni kubwa kwa hapa nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mafunzo hayo yamegawajika katika awamu mbili; awamu ya kwanza ina jumla ya vijana 20 ambao tayari wameishaanza mafunzo chuoni hapo ambapo  watapata mafunzo maalumu kwa muda wa miezi miwili. Mafunzo hayo yatahusisha kujifunza uchezaji ngoma za asili ya Tanzania, ngoma za ubunifu, muziki wa asili ya Tanzania, uigizaji, matumizi ya jukwaa na maleba.

Kwa awamu ya pili itahusisha vijana 7 ambao watapata mafunzo katika ngazi ya stashahada (diploma) na Astashahada (certificate) katika fani za Sanaa za maonyesho na ufundi (performing and visual arts).

Share:

Leave a reply