Dkt. Hamisi Kigwangalla aendelea na ziara mkoani wa Arusha

518
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla ametembelea Kituo cha Afya Momela kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo aliagiza kuhakikisha wanakifanyia marekebisho madogomadogo kwani kimejitoshereza na kina vifaa vya kutosha pamoja na wataalam.

Mbali na kituo hicho pia Dk. kigwangalla aliweza kutembelea vituo vya Afya kikiwemo cha USA River, Kituo cha Afya Mbuguni na kituo cha Afya Nduruma. Akizungumza wakati wa kutoa maagizo kwenye vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. Timothi Wonanji pamoja wasimamie wa vituo hivyo, kuhakikisha wanatatua changamoto za Afya kwenye vituo hivyo.

Aidha akitoa agizo wakati kukagua kituo cha Afya Mbuguni waanze kufanya huduma za upasuaji kwani wanavifaa vya kutosha na mtaalamu huku pia kuhakikisha wakaongeza mtaalam wa dawa za usingizi.ameagiza mara moja jengo la Chumba cha Upasuaji cha kituo hicho kianze kazi ndani ya wiki mbili na upasuaji ufanyike ikiwemo wataalamu kuwapo hapo muda wote.

“Naagiza ndani ya wiki mbili. Huduma za upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho kila kitu , vifaa vingi na vya kutosha na jengo zuri la kisasa,” alisema, Dk Kigwangalla.

Aidha katika ukaguaji huo, Dk. Kigwangalla ameweza kukagua sehemu za maabara, wodi za wazazi na vyumba vya upasuaji pamoja na maeneo mbalimbali ya hospitali kuona utendaji wa kazi muhimu na namna ya utoaji wa huduma.

Dk. kigwangalla ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara hiyo ya kikazi tayari ametembelea vituo vya Afya na Hospitali za mkoa wa Arusha zikiwemo wilaya za Longido, Arumeru, Arusha DC, Arusha mjini na maeneo mengine mbalimbali ya mkoa wa Arusha.

Share:

Leave a reply