Dkt. Kigwangalla akerwa na mifumo ya maji Hospitali ya Wilaya Korogwe, atoa maagizo mazito

279
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ametoa siku 60 kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga, kurekebisha miundombinu ya majitaka hususan wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji.

Alitoa  agizo hilo juzi baada ya kukagua shughuli za utaoji huduma, ikiwamo kushuhudia changamoto zinazowakabili.

Dk Kigwangalla alikumbana na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya majitaka, ambayo imekuwa kikwazo kwa utendaji wa watumishi na wagonjwa.

“Mfumo wa majitaka hapa hauko vizuri, ni hatari kwa afya zenu watumishi na wagonjwa, nawapeni siku 60 kuhakikisha mmefanyia marekebisho,” aliagiza.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Gwamaka Mwabulambo alimweleza Naibu Waziri huyo kwamba mwaka wa fedha wa 2016/17, zimetengwa Sh50 milioni kwa ajili ya ukarabati wa hospitali.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa alisema agizo hilo limetolewa wakati mwafaka kwani litasaidia kunusuru milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na aliahidi kulisimamia.

Tazama MO tv hapa:

DSC_0935

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni  wakati wa ziara yake hiyo katika Hospitali hiyo

DSC_0943 DSC_0946

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vyumba vya wodi ya watoto na akina maama

DSC_0947 DSC_0951Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa akitoa maagizo ya namna ya kufanyia marekebisho mfumo wa maji. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa.

DSC_0955

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akisikiliza kwa makini majibu ya Makandarasi wa Wilay  na anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa pamoja na maafisa wengine DSC_0938

DSC_0962

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akitoka kukagua maabara ya Hospitali hiyo

DSC_0967

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa akimfafanulia jambo 

DSC_0972

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akiongea na waandishi wa Habari alipotembelea (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog

Share:

Leave a reply