Dkt.Kigwangalla azifungia Hospitali za Wa-Korea zilizokuwa zikitoa huduma bila kibali Dar

365
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla  ameamuru kufungwa mara moja Hospitali mbili zilizokuwa zikiendesha huduma za matibabu mbalimbali kwa binadamu bila kuwa na vibali vinavyoelekeza ama kuruhusu kwa kutolewa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

Katika ziara maalum na ya ghafla katika Hospitali hizo ikiwemo ile ya Korea Midical Clinic Iliyopo katikati ya Jiji la Dar e Salaam katika Mtaa wa Mahiwa eneo la Kariakoo ambapo katika uvamizi huo Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliambatana na maafisa kadhaa akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo na wanahabari ambapo walikuta Raia wa Korea wakiendelea na Huduma  kwa wateja wao (wagonjwa) huku wakitoa huduma zingine zilizobainika kuwa hawana vibali vya kufanya hivyo.

Katika hali ya kushangaza, licha ya kubwana kwa raia hao wa Korea waligoma kuonyesha ushirikiano kwa msafara huo wa Naibu Waziri  hata hivyo baadae baada ya kuulizwa mambo ya kitaalam walishindwa kujibu wakidai kuwa hawaongei lugha ya kiswahili wala kiingereza.

Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla aliweza kubaini mapungufu mengi ikiwemo dawa ambazo hazikustahiri kuwapo katika Hospitali hiyo ikiwemo madawa makali ya usingizi na mengine mengi licha ya kuwa na kibali cha kutibu magonjwa ya ngozi, kibali ambacho walipewa pia kilikuwa ni cha muda.

“Nafunga na naagiza msajiri wa hospitali binafsi na baraza la tiba asili na tiba mbadala kumfungia mara moja mpaka hapo atakapokamilisha taratibu zote za usijali na nipate taarifa ndani ya siku saba nipate barua” alieleza Dk. kigwangalla.

Aidha, Katika eneo lingine ambalo Naibu Waziri Dk. Kigwangalla alivamia katika kuhakikisha watanzania wanapatiwa tiba sahihi na wataalam ambao wanafuata sheria na haki zilizowekwa, alifika katika Hospitali ya Oriental Traditional medicine clinic iliyopo eneo la Magomeni Mikumi Wilayani Kinondoni na kubaini Hospitali ambayo nayo inamilikiwa na Raia wa Korea wakifanya kazi za utoaji wa huduma pasipo kufuata taratibu za nchi ikiwemo vibali vya kuwaruhusu kufanya hivyo.

Katika hali ya kushangaza, Wakorea hao waligoma kabisa kuonyesha ushirikiano kwa Naibu Waziri kwa kile walichoeleza kuwa hawajui kuongea lugha ya Kiingereza wala kiswahili licha ya wao kutoa huduma hiyo kwa watanzania wengi ambao lugha yao ni kiswahili.

Katika kutembelea huko waliweza kukuta vifaa mbalimbali ambavyo vinaruhusiwa kwa wale wanaotoa huduma za tiba mbadala na tiba asili ambapo kwa upande wao wao walikuwa na vifaa mbalimbali huku wakichanganya huduma hizo zikiwa sambamba na zile zinazotolewa katika Hospitali nyingine.

Dk. Kigwangalla ameweza kuamuru kufungwa kwa Hospitali hizo za Wa-Korea ambazo zinaelezwa kuwa chini ya kampuni ya Maibong huku akiwataka kuhakikisha wanafuata taratibu zote muhimu za utoaji wa tiba hapa nchini pamoja na kuwa na vibali sahihi kaama vilivyoamuliwa na sheria ya utoaji wa tiba. 

Pia Dk. kigwangalla ameagiza ndani ya siku saba kwa wahusika wote kuhakikisha wanatekeleza upatikanaji wa vibali halali vinavyoruhusu kufanya kazi hizo ra sivyo wataendelea kuzifungia moja kwa moja.

Tazama MO tv kuona tukio hilo:

DSC_1054

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika eneo Hospitali ya Raia wa Korea, Korea Medical  Clinic iliyopo Mtaa wa Mahiwa Kariakoo

DSC_1059

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo (kulia) wakati wa kujiandaa kuingia katika Hospitali ya Wakorea ambayo imeamuriwa kufungwa kwa muda mpaka watakapotimkiza masharti ya ufanyaji wa kazi.

DSC_1062

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiingia katika hospitali hiyo ya wakorea.

DSC_1065 DSC_1073

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisoma moja ya vibali katika hospitali hiyo.

DSC_1075 DSC_1081 DSC_1086

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jaambo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo

DSC_1091

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo akitoa maagizo kwa mmoja wa raia wa Korea katika hospitali hiyo.

DSC_1096

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo akikagua moja ya maeneo ambayo yanadaiwa kuwana dawa zaidi ambazo hazitastaahili kuwapo katika hospitali hiyo.

DSC_1100

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangaia eneo la kuhifadhia dawa

DSC_1102

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya dawa zilizokutwa humo.

DSC_1108 DSC_1112

Eneo la kutolea matibabu.

DSC_1118

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuonyesha afisa mwandamizi wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala vifaa ambavyo vinatumika hapo wakati hawana vibali vya kutoa huduma hiyo.

DSC_1122

vifaa tiba na eneo la kutolea tiba.

DSC_1125

Vifaa tiba vya kisasa ambavyo wakorea hao wanavitumia.

DSC_1127

Mmoja wa viongozi wa Hospitali hiyo ya wachina akimuonyesha Naibu Waziri (hayupo pichani) namna vifaa hivyo vinavyofanya kazi.

DSC_1126 DSC_1133

Vifaa hivyo vilivyokutwa

DSC_1129DSC_1134

Madawa yaliyokutwa

DSC_1154

Magonjwa wanayotibu

DSC_1170

Wakionyesha magonjwa wanayotibu

DSC_1147

Vifaa hivyo vilivyokutwa

DSC_1141

Dk. Kigwangalla akipata maelezo kwa wakorea hao

DSC_1178

Dk Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza  kukagua hospitali hiyo na kutoaa maagizo ya kuifungia.

HOSPITALI YA WAKOREA YA MAGOMENI MIKUMI

DSC_1186 DSC_1187

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata huduma maara baada ya kuwasili katika hospitali ya wakorea ya Magomeni-Mikumi wakati wa ukaguzi huo

DSC_1190 DSC_1198

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya madawa yaliyokutwa kaatika hospitali hiyo

DSC_1205

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangaalia cheti  cha hospitali hiyo

DSC_1209

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla  akitoka katika Hospitali hiyo mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi huo mapema leo Aprili 15.2016.

Share:

Leave a reply