Dkt. Mwakyembe azitaka Simba na Yanga kuwa na viwanja vya mazoezi

141
0
Share:

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezitaka klabu za Simba na Yanga kujenga viwanja vyao vya mazoezi ili kuepusha lawama pindi wanapozuiliwa kutumia viwanja vya serikali.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na Gendarmerie ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 4-0, magoli yakifungwa na Said Ndemla, John Bocco ambaye alifunga magoli mawili na Emmanuel Okwi.

“Yanga ina umri wa miaka 83 Simba miaka 82 imefika kipindi sasa wawe vi viwanja vyao vya mazoezi vizuri vya kisasa, tusiendeleze maneno maneno wanapata gate collection inakwenda sijui wapi, wajenge viwanja sasa, miaka 83 kwa mtu mzima ni mzee kabisa, 82 ni mzee kabisa, timu zote tuzozisikia zina viwanja vyao,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, Dkt. Mwakyembe alipongeza kiwango ambacho kimeonyeshwa na wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga na Simba kwamba zimefanya vizuri na kuzitaka kufanya maandalizi mazuri ili katika michezo ya marudiano wafanye vizuri.

Share:

Leave a reply