Dkt Pepper kulipa Paunii 1.7 bilioni kununua nembo ya kampuni inayotishia uhai wa Coca na Pepsi

370
0
Share:

Dkt Pepper Snapple Group wananunua kampuni ya Bai Brands, moja ya aina ya maji kinywaji chenye ladha nzuri kinachotengeneza nchini Marekani, ununuzi ni kiasi cha Pauni za kiingereza 1.7 bilioni.

Dili hilo la ununuzi wa Bai itakuwa tishio kubwa la kibiashara kwa Coca-Cola na Pepsi, katika dili ambayo inaweza kupelekea kushuka kwa mauzo ya soda kutokana na tafiti mbalimbali za tishio la kiafya kwa watumiaji.

Tafiti mbalimbali za wanasayansi zinaonyesha kwamba matumizi ya soda yanaweza kuendelea kupungua kutokana na aina ya kemikali zinazotumika kutengeneza soda na kutokana na tafiti hizo kampuni hiyo ya maji inaweza kutengeneza faida kubwa ya kibiashara.

Kampuni hiyo ya Bai ilitengeneza faida ya kiasi cha Pauni za kiingereza 120 milioni kama mauzo mwaka jana, mwaka huu mauzo yanaweza kuongezeka maradufu kufikia Pauni za kiingereza 300 milioni.

justin-timberlake

Justin Timberlake.

Kampuni hiyo ya Bai inatarajiwa kukua zaidi mwaka ujao baada ya ujio wa ununuzi huo anasema msemaji wake, Justin Timberlake.

Timberlake anajiunga na kampuni hiyo ya Bai kama mwekezaji na Afisa mtendaji mkuu wa kampuni, kampuni hiyo ilitangaza mwezi uliopita.

Amesema kwamba atatumika kiasi cha Pauni za kiingereza 100 millioni katika kutangaza zaidi bidhaa hiyo kupitia kitengo cha masoko ambapo kampuni hiyo itazinduliwa rasmi mwakani 2017.

Share:

Leave a reply