Dkt. Tulia Ackson akabidhi TV sita JKCI

69
0
Share:

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) akabidhi runinga sita (6) kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto. Awajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwajulia hali mapacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu. Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto.
Picha na JKCI

Share:

Leave a reply