Donald Trump aendeleza vita na waislamu

306
0
Share:

Mgombea urais wa Marekani kwa kupitia tiketi ya Republican, Donald Trump anaonekana kuendeleza vimbwanga kila ku kicha, katika kampeni zake za kuwania kiti cha urais nchini humo.

Trump ambae amekua akiwaomba wamarekani kumpa kura ili aweze kurudisha hadhi ya nchi hiyo kwa kuimarisha hali ya kiuchumi na kuiweka katika hali salama kwa kupambana na ugaidi wa waislamu wenye itikadi kali.

Amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa Marekani atabadilisha sera za mambo ya nje ya nchi hiyo yenye lengo la kujenga taifa kwa kuwa na sera zanye uhalisia.

Akihutubia mkutano wake katika jimbo la Ohio, mgombea huyo alisisitiza juu ya umuhimu wa mpango wa muda wa kuzuia viza za waombaji wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya kueneza ugaidi na kupendekeza kuanzishwa kwa mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Aidha Trump ameonesha nia ya kuwa tayari katika kushirikiana katika kazi na nchi yeyote ile bila kujali tofauti za kiitikadi lakini akiwa na nia ya kusaidia kulitokomeza kundi la Islamic State (IS).

Chanzo: BBC Swahili

Na Laudanus Majani – UDSM – SJMC

Share:

Leave a reply