Doris Mollel Foundation yatoa msaada wa mashine 3 za kusafishia njia ya hewa kwa watoto

262
0
Share:

Doris Mollel Foundation ikishirikana na Commercial Bank of Africa (CBA ) wamekabidhi vitanda viwili vyaa kuzalia na machine 3 za kusafisha njia ya hewa kwa watoto njiti.

Meneja Mahusiano wa CBA, Caroline Makatu alisema wao kama wanawake wa CBA wameamua kuwakumbuka watoto hao pamoja na wamama wajawazito kwenye siku hiyo muhimu kwa wanawake.

“Watoto njiti ni watoto wanaopitia shida katika ukuaji wao hivyo tumeamua kuunga jitihada za Doris Mollel Foundation kwa kuwawekea mazingira bora,” alisema Makatu.

Aidha siku hiyo ambayo ilisindikizwa na ufanyaji usafi katika wodi za pre-mature katika hospital ya Amana, Muhimbili, Mwanayamala, KCMC Moshi na Bugando ya Mwanza.

Kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa hospitali, Doctor Delilah Moshi ameishukuru taasisi ya Doris Mollel na CBA kwa msaada huo ambao wamewapatia.

Doris Mollel Foundation

Meneja Mahusiano wa Benki ya CBA, Caroline Makatu (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa vitanda na mashine kumsaidia mtoto anayezaliwa kabla ya muda, kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Delilah Moshi, katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo, jijini Dar es Salaam.

Doris Mollel Foundation

Daktari akimuhudumia mtoto.

2

Baadhi ya Maafisa kutoka Benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja wadau waliofanikisha msaada huo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply