DStv,Waziri Nape wamkabidhi Diamond bendera ya Taifa, kutumbuiza AFCON 2017

659
0
Share:

Ili kuwapa watanzania wengi uhakika wa kushuhudia michuano ya kombe Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017, kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi chake maarufu cha DStv, itaonyesha michuano hiyo katika kifurushi chake cha bei ya chini kabisa maarufu kama DStv Bomba.

Kifurushi hicho kinachopatikana kwa bei ya shilingi 19,975 tu, ni miongoni mwa vifurushi vya bei nafuu katika huduma ya ving’amuzi hapa nchini.

Akizungumza katika  tukio maalum la kukabidhiwa bendera  leo 11 Januari 2017, kwa Mwanamuziki wa kizazi kipya hapa nchini Nasibu Abdul (Diamond) ambaye anaenda kupiga shoo katika ufunguzi wa mashindano ya AFCON 2017, nchini Gabon,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Multichoice Tanzania Salum Salum, ametanabahisha kuwa  kupitia  king’amuzi pekee cha DStv,  kitaonyesha michuno hiyo mubashara kupitia chaneli yake ya michezo ya SuperSport4 (DStv 204).

Ambapo amesema wameamua kuiweka michuano hiyo kwenye kifurushi cha bei nafuu kabisa cha Bomba, ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kuiona michuano hiyo moja kwa moja.

“Tunajivuna kuwa na sisi Tanzania tumepiga hatua kubwa sana na sasa hatuna sababu yoyote ya kuona michezo iliyerekodiwa, bali na sisi tunaitazama mubashara kupitia king’amuzi chetu bora cha DStv, tena kwenye kifurushi nafuu cha Bomba” alisema Salum na kuongeza kuwa kwa kuwa hii itawapa nafasi watanzania wengi kufurahia michuano hiyo kila mahali ikiwemo kwenye kumbi za burudani na hata majumbani.

 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Multichoice Tanzania Salum Salum akielezea taarifa namna DStv wanavyoshirikiana na wadau wengine wakiwemo Serikali katika masuala mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwapa mambo mazuri wateja wao wa ving’amuzi hivyo vya DStv hapa nchini.

Kwa upande wake,  Wizara ya Habari Utamaduni Michezo na Sanaa, imefanikisha safari ya Mwanamuziki wa kizazi kipya hapa nchini,  Nasibu Abdul (Diamond) katika kufanikisha onyesho lake katika ufunguzi wa mashindano ya AFCON nchini Gabon.

Diamond ni miongoni mwa wasanii teule watakaotumbuiza katika hafla hiyo kitendo ambacho kimechukuliwa na watanzania wengi kuwa ni fursa ya Tanzania kusikika katika mashindano hayo japokuwa timu yetu haikuweza kufuzu kushiriki.

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Mh. Nape Nnauye amesema kuwa, kuwepo kwa Diamond kwenye uzinduzi wa michuano hiyo ni kitendo cha kujivunia na kwamba Serikali ikishirikiana na DStv imefanya jitihada kubwa kufanikisha safari ya WCB kuelekea Gabon.

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Mh. Nape Nnauye akizungumza wakati wa tukio hilo

Naye  msanii  Diamond aliishukuru Serikali na DStv kwa ushirikiano wao hususan kufanikisha safari yao ya kuelekea Gabon. Aliongeza kuwa jitihada binafsi za Waziri wa Habari ziliwezesha zoezi hilo kufanikiwa na kwamba wanaahidi kuwa hawaendi kama WCB, bali kama watanzania na watahakikisha kuwa wanaipeperusha vema bendera ya Tanzania katika onyesho hilo.

Msanii  Diamond akiishukuru DStv na Serikali kwa kufanikisha tukio lake hilo la kwenda kutumbuiza katika michuano hiyo ya AFCON 2017.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph amebainisha kuwa,  vifaa vya DStv vinapatikana sehemu mbalimbali hivyo wananchi wajitokeze kwa wingikuvinunua pamoja na kupata kulipia malipo yao ilikushuhudia michuano hiyo iliyojaa uhondo wa kila aina ambapo kwa mwaka huu michuano ya AFCON inanogeshwa zaidi na uwepo wa wachezaji nguli ulimwenguni hususan wale wanaochezea vilabu vikubwa

Vikiwemo Manchester United, Arsenal, Chelsea, Real Madrid na vilabu vingine vikubwa duniani. Wababe wa kabumbu kama Mohamed Elneny, Eric Bailly, John Obi Mikel, Pierre Aubemayang, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Victor Moses ni miongoni mwa vigogo watakaoonyesha umahiri wao katika michuano hiyo.

Mtifuano huo wa AFCON mwaka huu unafanyika katika nchi ndogo ya Gabon, huku jumla ya timu 16 zikishiriki ikiwemo Uganda ambayo ndiyo timu pekee iliyofuzu kutoka Afrika Mashariki.

 

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph akizungumza katika tukio hilo.

Tayari vuguvugu la michuani hiyo limeshaanza kushika kasi mitaani ambambo mashabiki wa timu mbalimbali wamekuwa wakitambiana kila mmoja akidai timu yake itanyakua ubingwa mwaka huu.

Michuona ya AFCON 2017 inadhaminiwa na kampuni ya Total, na itaanza tarehe 14 January na fainali itakuwa tarehe 05 Februari. Tayari ratiba kamili ya michuano hiyo imeshatolewa na inapatikana katika tovuti ya www.dstv.com.

 

Vijana wanaopiga nyimbo za Asili za kabila la Wasafwa kutoka Mkoa wa Mbeya, wakifahamika kama ‘MWIDUKA BAND’, wakitoa burudani katika tukio hilo.

Waziri Nape akijadiliana jambo meza kuu akiwemo Balozi wa DStv, msanii mchekeshaji Joti pamoja na Bw. Salum Salum

Waziri Nape akisalimiana na Msanii Diamond 

Dada Shumbana wa DStv akifungua tukio hilo

Msanii Joti ambaye ni Balozi wa DStv akitoa neno katika tukio hilo

Msanii Diamond akizungumza katika tukio hilo

Msanii Diamond akiwa na bendera ya Tanzania baada ya kukabidhiwa

Waziri Nape akimkabidhi bendera Diamond. Katikati ni Balozi wa DStv msanii Joti

Waziri Nape akikabidhi bendera kwa Diamond

Wanahabari wakichukua matukio katika tukio hilo

Diamond akiwa na bendera ya Tanzania baada ya kukabidhiwa.

Share:

Leave a reply