Duka la nguo la Woolworths lawazawadia washindi wawili vocha za manunuzi

476
0
Share:
Woolworths Tanzania

Wateja wawili wa duka la nguo la Woolworths Ashura Waijaa wa Dar es Salaam na Moris Nyangabo  wa Arusha wameibuka washindi katika droo ya mwezi Februari iliyochezeshwa na duka hilo ambapo kila mmoja amejishindia vocha yenye thamani ya shilingi laki tano itakayowawezesha kufanya manunuzi katika maduka ya Woolworths.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vocha yake, Ashura alisema amefurahia kuwa mmoja kati ya washindi wawili na kuongeza kuwa vocha hiyo itamwezesha kununua nguo kwa ajili yake pamoja na familia yake.

Wakati napigiwa simu kuambiwa kuwa nimeshinda, ilikuwa vigumu kuamini  kuwa kweli  nimeshinda, nilidhani ni matapeli ambao  hutumia mbinu mbali mbali ikiwamo kuwapigia watu simu na kuwadanganya wameshinda ili kujipatia fedha kwan njia za udanganyifu,” alisema.

 Woolworths Tanzania

Mkurugenzi wa Fedha wa duka la nguo la Woolworths Tanzania, Samson Katemi ( Kulia) akishuhudia mfanyakazi wa kampuni hiyo Mary Stanford (kushoto) akimuonyesha mzigo mpya Ashura Waijaa ( katikati) ambaye ni mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya mwezi Februari 2016 iliyoendeshwa na duka hilo. Ili mteja aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na kadi maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Bi Ashura aliwashauri akina mama na watanzania kwa ujumla kununua nguo zenye ubora katika maduka ya Woolworths ili pia kujitengenezea nafasi ya kushinda vocha zitakazowawezesha kununua kwa ajili yao na familia zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha wa duka hilo Samson Katemi alisema mteja yeyote mwenye kadi ya manunuzi (WReward Loyalty card) anayo nafasi ya kushinda vocha ya manunuzi katika droo ambazo huchezeshwa kila mwezi.

Mkurugenzi huyo wa fedha aliwataka watanzania kutembelea maduka ya Woolworths ili kupata bidhaa zenye ubora wa kimataifa haswa katika msimu huu wa sikuu ya Pasaka ambapo mzigo mpya kwa ajili ya sikukuu umeingia.

 Woolworths Tanzania

Mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya mwezi Februari 2016 iliyoendeshwa na duka la Woolworths,Ashura Waijaa, akichagua viatu katika Duka la Woolworths baada ya kujishindia vocha yenye thamani ya shilingi Laki Tano ambayo itamwezesha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths. Ili mteja aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na kadi maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

 Woolworths Tanzania

Mfanyakazi wa Duka la Woolworths Mary Stanford akimjaribisha viatu mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya mwezi wa Februari 2016 Ashura Waijaa, baada ya kujishindia vocha yenye thamani ya shilingi Laki Tano ambayo itamwezesha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths. Ili mteja aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na kadi maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths (Wreward Loyalts Card) Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

 Woolworths Tanzania

Mkurugenzi wa Fedha wa maduka ya nguo ya Woolworths Samson Katemi, akimshuhudia mshindi wa droo ya Mwezi Februari 2016, Ashura Waijaa akisaini fomu maalum baada ya kuibuka mshindi wa vocha yenye thamani ya shilingi laaki tano ambayo itamwezesha kununua bidhaa katika maduka hayo. Ili mteja aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na kadi maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

 Woolworths Tanzania

Mkurugenzi wa Fedha wa maduka ya nguo ya Woolwoorths Tanzania, Samson Katemi ( Kulia) akimkabidhi vocha zenye thamani ya shilingi Laki Tano mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya mwezi wa Februari 2016,Ashura Waijaa ( kushoto), baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo iliyoendeshwa na kampuni hiyo. Ili mteja aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na kadi maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) . Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

003 w

Mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya mwezi Februari 2016 inayoendeshwa na duka la nguo la Wooworths , ambaye ni mkazi wa jijini Arusha Moris Nyangabo, akikabidhiwa vocha yenye  thamani ya shilingi laki tano ambayo itamwezesha kununua bidhaa katika maduka ya Woolworths na Meneja Masoko wa duka hili Edwina Barongo. Ili mteja  aweze kushiriki katika droo hiyo anahitajika kuwa na  kadi  maalumu ya kumwezasha kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card)  Hafla hiyo ilifanyika jijini jana.

Share:

Leave a reply