EasyJet yapigwa faini kwa kuzuia mlemavu kupanda kwenye ndege

610
0
Share:

Kampuni ya ndege ya EasyJet imepigwa faini ya Pauni 52,000 na mahakama nchini Ufaransa kwa kukutwa na hatia ya kumzuia abiria ambaye ni mlemavu kuingia ndani ya ndege kwa sababu ya usalama wa mtu huyo.

Mahakama ya Bayonne imeipiga faini EasyJet kwa kumzuia Joseph Etcheveste (55) kusafiri Julai, 2010 kwa kisingizio kuwa abiria huyo hakuwa na mwangalizi jambo ambalo ni hatari kwake kama lingetokea tatizo wakati wa safari.

“EasyJet ilikataa kumruhusu mteja wangu kwasababu ya hofu ya matatizo ya kiusalama, lakini bado wanashindwa kueleza wao walikuwa wapi,” alisema wakili wa Joseph, Anne-Marie Mendiboure kabla ya hukumu haijatolewa.

Hii sio mara ya kwanza kwa EasyJet kupigwa faini kwani Desemba, 2015 walipigwa faini ya Euro 70,000 kwa kukataa watu watatu wenye matatizo ya akili wasiingie katika ndege kwa sababu hiyo hiyo kama waliyotoa kwa Joseph kuwa ni sababu za kiusalama.

Share:

Leave a reply