Emirates yaongeza muda wa nauli maalum za Dubai na ofa ya viza bure

1169
0
Share:

Kampuni ya ndege ya Emirates imeongeza muda wa ofa kwa wasafiri kutoka Tanzania kwenda Dubai kwa ofa maalum ndani ya daraja la kawaida na daraja la juu kwenye nauli ya kwenda na kurudi ambayo itaambatana na viza bure, nafasi ya kuweka mzigo usiozidi kilo 23 na My Emirates Pass.

Katika ofa hiyo maalum, tiketi ya daraja la kawaida kutoka Dar Es Salaam mpaka Dubai ni USD 399 na daraja la juu ni USD 1999. Ofa hiyo ya nauli inatengemea na uwepo wa nafasi, vigezo na masharti na kwa muda ulioainishwa tu. Unaweza kutuma maombi ya kupata nafasi kati ya 11 Julai na 24 Julai wakati safari ni kati ya 11 Julai na 30 Novemba 2017. Gharama ya tiketi inajumuishwa pia na kodi ya uwanja wa ndege.

Emirates pia inatoa ofa ya viza ya siku 30 ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (inatengemea na uthibitisho wa idara ya uhamiaji), nafasi ya kuhifadhi mzigo isiozidi kilo 23 kwa daraja la kawaida na mpaka kilo 32 kwa daraja la juu, vile vile My Emirates Pass inaweza kutumika kwa ofa mbalimbali na kupata punguzo ndani ya Dubai.

My Emirates Pass ambayo inatumika mpaka 31 August 2017, inawapa wateja punguzo maalum katika mahotel na migahawa zaidi ya 120 yenye ubora duniani ndani ya Dubai. Pia kuna ofa mbalimbali katika nyanja ya burudani, kutembelea shindano la gofu, kutembelea mbuga na sehemu maridhawa ndani ya jiji la Dubai.

Wageni wakiwa huko wanaweza kutumia My Emirates Pass kufurahia vivutio vya jiji na sehemu maarufu kama Hifadhi ya Dubai na mwambao ikiwemo na hifadhi tatu maarufu kama bollywood, Dubai Motiongate bila kusahau hifadhi ya kwanza katika mkoa huu legoland park na legoland water park.

Ndege za Emirates zinasafiri mara moja kila siku kati ya Dubai na Dar Es Salaam ikitumia Boeing 777.

Share:

Leave a reply