EU yaipatia Tanzania mabilioni ya pesa kusaidia sekta ya kilimo

61
0
Share:

Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia serikali ya Tanzania msaada wa Euro Milioni 4.5 (Tsh. 12 Bilioni) ili kufanikisha miradi mikubwa mitatu ya sekta ya kilimo ambayo inatekelezwa kupitia Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Iringa, Morogoro ambapo itafanyika miradi miwili.

Akizungumza kuhusu msaada huo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa alisema msaada huo utasaidia wakulima wadogo kuboresha kilimo chao na kuwa cha kibiashara zaidi kuliko sasa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa akizungumza kuhusu msaada wa Euro Milioni 4.5 (Tsh. 12 Bilioni) uliotolewa na Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Tanzania.

Mwanjelwa alisema pamoja na kuwanufaisha wakulima, pia kama nchi itanufaika kutokana na biashara itakayokuwa ikifanyika jambo ambalo litasaidia uchumi wa nchi kukua.

“Wamekusudia kufufua kilimo cha kisasa, kilimo bora ili Watanzania wanufaike na kilimo kwa kuwa na soko. Faida yake ni upatikanaji wa chakula, lishe na biashara na mwisho wa siku wananchi wote wanufaike,” alisema Mwanjelwa.

Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van de Geer alisema EU imedhamiia kusaidia mirad mingi hapa nchini katika sekta ya chakula ili kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inakuwa na chakula cha kutosha.

Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van de Geer akizungumza kuhusu msaada wa Euro Milioni 4.5 (Tsh. 12 Bilioni) uliotolewa na Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Tanzania.

 

 

 

Share:

Leave a reply