EU yatangaza majina 15 ya washiriki shindano al European Youth Film 2017

490
0
Share:

Umoja wa Ulaya (EU) nchini umetengaza majina ya watu 15 ambao wamesonga mbele kwenye shindano la European Youth Film 2017 ambalo limeandaliwa na umoja huo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Ujerumani na Serikali ya Tanzania.

Washiriki ambao wamefuzu ni Christine Pande, Cornel Mwakyanjala, Daniel Manege, Dennis Chacha, Dosi Said Dosi, Florence Mkinga, Francis Nyerere, Franch Machiya, Freddy Feruzi, Karim Michuzi, Kherry Kafuku, Louis Shoo, Malik Hamis, Rashid Songoro, Taragwa Marwa na Wambura Mwikabe.

Akizungumza kuhusu shindano hilo, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland van de Geer alisema washiriki hao 15 wamechaaguliwa kutoka na filamu walizotengeneza na kuwa lengo la kuanzisha shindano hilo ni kuiwezesha Tanzania kuwa na watengeneza bora wa filamu.

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland van de Geer akizungumza kuhusu shindano la European Youth Film 2017.

“Kabla ya kuanza kutengeneza filamu walipewa mafunzo ya siku tatu kuhusu kutengeneza filamu, lengo ni Tanzania iwe na filamu bora sio kuleta filamu kutoka Ulaya ila kuboresha filamu za Tanzania kupitia vijana ambao ndiyo sehemu kubwa ya Watanzania,” alisema Geer.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Bodi ya Filamu nchini, Wilhadi Tairo alisema shindano hilo limekuja kwa wakati mwakafaka kwani ili soko la filamu liwe imara linahitaji kuwa na watu wa aina zote wenye uwezo wa kushiriki nafasi zote za kwenye filamu.

“Filamu zinahusisha watu wa aina zote awe mtoto au mkubwa na kama hakuna watu wa aina zote hapo kutakuwa na upungufu kwahiyo mimi washukuru Umoja wa Ulaya pamoja na washirika wao kwa kuleta shindo hili kwa muda mwafaka,” alisema Tairo.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Bodi ya Filamu nchini, Wilhadi Tairo akizungumza kwa upande wa Serikali kuhusu shindano European Youth Film 2017.

Shindano hilo la European Youth Film 2017 linatarajiwa kumalizika mwezi Septemba na mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya milioni saba (7), mshindi pili milioni tano (5) na mshindi wa tatu milioni tatu (3).

Share:

Leave a reply