Everton yamchukua kocha wa Southampton, Ronald Koeman

227
0
Share:

Tetesi zilizokuwa zikisambaa kwa siku kadhaa zimekamilika za kocha wa Southampton, Ronald Koeman kuhamia Everton na kuchukua nafasi iliyoacha wazi na Roberto Martinez baada ya kutimuliwa kazi.

Makubaliano ya Koeman kuhamia Everton tayari yameshafanyika na ili kukamilisha dili hilo Everton inatakiwa kuilipa Southampton kitita cha Pauni Milioni 5 ili kumwachia kocha huyo ambaye alijiunga Southampton mwaka 2014.

Kujiunga kwa Koeman kukinoa kikosi cha Everton anataraji kulipwa kiasi cha pesa cha Pauni Milioni 6 kwa mwaka na kupatiwa Pauni Milioni 100 kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha klabu hiyo.

Share:

Leave a reply