Facebook yafikisha watumiaji bilioni mbili

660
0
Share:

Matumizi ya mitandao ya kijamii inazidi kuongezeka duniani na watu mbalimbali wakitumia kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki ambao wapo sehemu mbalimbali iwe ni karibu au mbali na wanapoishi.

Mtandao wa kijamii wa Facebook umaarufu wake unazidi kuongezeka kila siku zinavyozidi kwenda na Juni, 27 mtandao huo umeweka historia kwa kufikisha watumiaji bilioni mbili ambayo ni zaidi ya robo ya watu waliopo duniani.

Taarifa ya Facebook kufikisha watumiaji bilioni mbili ilitolewa na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg kupitia ukurasa wake wa mtandao huo kwa kuandika,”Asubuhi hii jamii ya Facebook imefikisha watu bilioni mbili.”

Idadi ya watu bilioni mbili imekuja ikiwa imepita miaka mitano tangu Facebook ilipotangaza kufikisha idadi ya watumiaji bilioni moja na pamoja na idadi kufika bilioni mbili bado idadi ya watu ambao wanajiunga inaonekana kuzidi kuongezeka kwa kasi.

Hata hivyo licha ya mafanikio hayo Facebook inatajwa kuwa mtandao wa kijamii wenye watumiaji wengi zaidi kuliko hata Instagram na Twitter.

Share:

Leave a reply