Fainali ya ASFC kati ya Simba na Mbao kuchezwa Dodoma Mei 28

958
0
Share:

Mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD – ASFC), kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, utafanyika Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Timu hizo zimeingia katika fainali ya kombe hilo ambapo kwa Simba SC iliweza kuiondosha AZAM FC kwa bao mmoja mchezo uliochezwa  Jijini Dar es Salaam huku Mbao wao wakifanikiwa kutinga fainali kwa kuwafunga Wanajangwani Klabu ya Yanga, kwa bao moja bila.

 

Share:

Leave a reply