Fedha za mchezo wa Ngao ya Jamii Yanga dhidi ya Azam FC kwenda kununulia madawati

256
0
Share:

Mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Magwiji wa soka Azam Fc na Yanga Fc inayotarajiwa kuchezwa hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam inatarajiwa kunufaisha wanafunzi wa shule ambao watapata mgao  wa madawati kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jacob Ndugai

Afisa habari wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Alfred Lucas amesema kuwa TFF kwa kushirikiana na Kampuni kusambaza ving’amuzi vya Ting itarusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi hiyo ya Ngao ya Jamii kati ya Azam Fc na Yanga Fc.

“Ting wamepata haki ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya kesho kama ambavyo huwa wanarusha matangazo ya mechi ya ligi za Uingereza “ amesema Alfred

Aidha Afisa habari huyo ameongeza na kusisitiza juu ya suala la Shirikisho la Mpira wa Miguu kufaidika na mtanange huo wa kesho wa Ngao ya Jamii.

“TFF haijalenga kupata mapato ya kesho kwenye Ngao ya Jamii kwaajili ya mpango wowote wa maendeleo ya Shirikisho, ila tumelenga kuisaidia na kuipa ‘support’Serikali katika mpango wake wa kusambaza madawati kwa shule za msingi ili wanafunzi wasikae tena chini, na kwa upande wetu TFF tunatoa madawati 200”. Ameongeza Alfred

 Mkurugenzi wa Michezo kutoka Kampuni ya Ting Bw. Dennis Msemwa ameomba wadau kuhudhuria mchezo huo wa ngao ya jamii

“Sisi kupitia king’amuzi cha Ting na ATN tunawaomba wadau wote wa Michezo na Vyombo vya Habari kujumuika nasi pale uwanja wa Taifa kuanzia saa kumi jioni, tunahitaji ushirikiano wetu wa hali na mali. Sisi ajenda yetu kubwa ni michezo, na michezo kwetu ni utamaduni na hii ndio kauli mbiu yetu” Amesema Dennis.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

DSC_5882Afisa Habari wa TFF, Bwana Alfred Lucas (kushoto) akielezea kuelekea mchezo huo wa Ngao ya Jamii ambao unachezwa kesho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Michezo wa TINGS, ambao ni wasambazaji wa ving’amuzi hivyo vya TINGS, Bwana Denis Msemwa.

 DSC_5889Mkurugenzi wa Michezo wa TING, ambao ni wasambazaji wa ving’amuzi hivyo vya TING, Bwana Denis Msemwa akizungumzia tukio hilo la wao kuingia mkataba na TFF kwa ajili ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

Share:

Leave a reply