Fidel Castro ajitokeza hadharani akisherekea kutimiza miaka 90

263
0
Share:

Kiongozi Mwanamapinduzi wa Cuba Bw. Fidel Castro amewashukuru wananchi wa Nchi hiyo kwa kumtakia kheri ya siku yake ya kuzaliwa pamoja na kumkosoa rais wa marekani Barack Obama kupitia barua yake ndefu aliyoichapisha kwenye vyombo vya habari.

Taarifa zinasema kuwa kiongozi huyo mwandamizi amejitokeza hadharani kusherekea siku hiyo ambapo inadaiwa kuwa awali kiongozi huyo alikuwa hajaonekana hadharani kwa miezi kadhaa na kwamba hadi sasa haijabainika iwapo atajitokeza siku za hivi karibuni.

Serikali ya Cuba iliandaa sherehe rasmi ya kumpongeza Castro na mmmoja wa wageni walihudhuria ni rais wa taifa la Venezuela ambalo ni mshirika wa karibu wa kisiwa cha Cuba, Bw. Nicolas Maduro aliwasili mjini Havana kushiriki katika sherehe ya Castro.

Katika barua yake Castro alieleza kuwa salamu za kheri alizopewa na wanacuba zimemfanya kuimarika kiafya.

Alisema wataalam wa afya wanaompa matibabu wamemwambia kuwa anaendelea vizuri.

Castro alikitawala kisiwa cha Cuba kwa zaidi ya miaka 50, alilazimika kuachia madaraka miaka 10 iliyopita baada ya kusumbuliwa na marathi.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply