FIFA yaipa tano TFF

153
0
Share:

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino amemshukuru Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Wallace Karia kwa kazi nzuri ya maandalizi ya mkutano wa FIFA wa maendeleo ya mpira (FIFA Football Executive Summit) uliofanyika Februari 22, 2018 Dar es Salaam,Tanzania.

Infantino ametoa pongezi hizo katika barua yake aliyomuandikia Rais wa TFF Karia, amesema wameondoka na kumbukumbu zisizosahaulika kuhusu Tanzania ikiwemo urafiki uliojengeka wakati wote waliokuwepo Tanzania.

Katika hatua nyingine Infantino ameridhishwa na utendaji kazi wa TFF tokea Karia ameingia madarakani pamoja na Kaimu Katibu Mkuu na kuwataka kuendelea kusimamia mpira katika utaratibu stahiki wenye uwazi kama wanavyofanya sasa.

Amesema FIFA kwa pamoja wameridhishwa na maandalizi na shughuli zote za mkutano huo na wamepokea mrejesho chanya kutoka kwa wajumbe wote waliohudhuria.

Share:

Leave a reply