Filamu 132 kuoneshwa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi ZIFF 2017

470
0
Share:

Uongozi wa  waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), mapema leo Mei  19.2017, wametangaza rasmi filamu zilizochaguliwa kwa mwaka huu na ambazo zitaoneshwa kwenye tamasha hilo msimu wa 20, hapo Julai  8-16-2017 katika viunga vya Ngome Kongwe, Unguja Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijii Dar e Salaam, Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo  amesema kuwa,  jumla ya filamu 132, zimeweza kuchaguliwa kuingia kwenye tamasha hilo.

“Jumla ya filamu 600,zilitumwa kwetu ZIFF kutoka nchi 70, Duniani kote. Lakini katika hizo, filamu 132 ndizo tulizozichagua na zitapata kuoneshwa kwa mwaka huu pale Ngome Kongwe, Zanzibar.

Katika filamu hizo 132, filamu 23 zinatoka Tanzania. Lakini pia zikiwa zimegawanyika katika aina mbalimbbali ikiwemo filamu ndefu, filamu fupi, filamu za katuni, na filamu zingine nyingi huku pia mwaka huu tumepata filamu kutoka nchini Namibia” ameeleza Mkurugenzi  huyo Colombo.

Kwa upande wake Meneja wa ZIFF, Daniel Nyalusi amebainisha kuwa, katika filamu hizo 23 kutoka Tanzania zimeweza kukidhi vigezo  hivyo kuoneshwa kwake ZIFF mwaka huu zitaongeza ufanisi na soko la filamu za Tanzania licha ya kuwa na changamoto  nyingi ikiwemo kukosa soko la ndani kutokana na  na nyingi kuandaliwa kwa bajeti ndogo, kukosa ubunifu katika uandishi wa stori na mengine mengi.

 “Soko la filamu linakua na zinaanza kuwa nzuri, lakini wingi wa uzalishaji umepungua. Ukosefu wa bajeti unapelekea wataarishaji kushindwa kutengeneza filamu zenye ubora na viwango vya kimataifa. Pia ukosefu wa ubunifu wakati wa uandishi wa stori nako pia kuna sababisha filamu zetu kukosa ubora,” amesema na kuongeza.

“Watunzi wetu wanaona lazima watunge stori zinazohusu mapenzi ndio zitanunulika, inabidi wabadilike namna ya uandishi pia tukubali kuongeza elimu na kuzitengeza filamu kulingana na bajeti iliyopo. Angalie filamu ya Kiumeni, ni ya bongo movie lakini ina stori tofauti sababu ya ubunifu wa hali ya juu uliotumika.”

Amesema ili kuondoa ukata wa fedha za kutengenezea filamu zilizo bora, wasanii inabidi wawashawishi wadhamini mbalimbali kudhamini filamu zao kama zinavyofanya nchi zilizoendelea.

“Kwenye filamu unakuta msanii anakunywa bia ya safari, anaitangaza ila watengenezaji bia hiyo hawawalipi. Lakini nchi za wenzetu wasanii wanatumia filamu kutangaza bidhaa zao. Lazima wakubalia kuanza tabia ya kushawishi wadhamini katika filamu zetu,” amesema.

Tamasha la ZIFF mwaka huu 2017, ni la 20, tokea kuanzishwa kwake na ufanyika kila mwaka  katika viunga vya Ngome Kongwe, Unguja ambapo limekuwa likiwakutanisha watu mbalimbali kutoka pembe za Ulimwengu wakijumuika pamoja na kushuhudia filamu mbalimbali zikioneshwa sambamba na uwepo wa Makongamano, Warsha, biashara, mafunzo kwa Jamii, Pia uwepo majukwaa ya  Watoto, Wanawake (Panorama) pamoja na Muziki kutoka kwa vikundi na bendi mbalimbali za ndani na nje.Meneja wa ZIFF, Daniel Nyalusi akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza filamu zilizochaguliwa mwaka huu katika msimu wa 20. mapema leo Mei 19.2017, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo akifuatiwa na Afisa Masoko na Mawasiliano kwa Umma wa ZIFF, Bi. Lara Preston

Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo  akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) mapema leo Mei 19.2017, Jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza filamu zilizochaguliwa mwaka huu kwenye tamasha hilo. Kushto ni Afisa Masoko na Mawasiliano kwa Umma wa ZIFF, Bi. Lara Preston 

Afisa Masoko na Mawasiliano kwa Umma wa ZIFF, Bi. Lara Preston akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) juu ya tamasha hilo la ZIFF msimu huu wa 20.  Mapema leo Mei 19.2017, Jijini Dar es Salaam

Share:

Leave a reply