Filamu, burudani zaendelea kwenye tamasha la 20 la ZIFF, Zanzibar

243
0
Share:

Leo Julai 10,2017 ni siku ya tatu ya tamasha la kubwa la Kimataifa la Filamu za nchi za Majahazi (ZIFF) tayari filamu na vikundi vya ngoma na wasanii mbalimbali wameendelea kutoa burudani katika tamasha hilo ambalo linatarajia kufikia tamati Julai 16,2017.

Tokea kuanza kwa  ZIFF, Zanzibar na viunga vyake ikiwemo Unguja imeendelea kuwa na pilipila za hapa na pale huku wageni na raia wa kigeni wakizidi kuongezeka kulishuhudia tamasha hilo lenye jumla ya filamu zaidi ya 120, ambazo zinaonyeshwa kila siku mpaka tamati hapo Julai 16,2017.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi ‘Dean’ amebaainisha kuwa, watu mbalimbali wameendelea kumiminika na kushuhudia filamu hizo zinazoonyeshwa kwenye maeneo tofautitofauti ya viunga vya Unguja huku nyingine zikioneshwa ndani ya Ngome Kongwe kuaanzia jioni.

“Tuna filamu zaidi ya 120. Filamu hizi zinaonyeshwa kwenye maeneo tofauti tofauti. Zipo zinazooneshwa katika hoteli yam ARU Maru, Double tree by Hilton  na maeneo mengine” alieleza Dean.

Aidha amebainisha kuwa, mara baada ya filamu kuisha ndani ya Ngome Kongwe, burudani inaamia upande wa pili wa Mambo Klabu ambapo vikundi vya Ngoma,  bendi na wasanii mbalimbali wataendelea na burudani.

Vikundi vya ngoma vikitoa burudani katika tukio liliofanyika usiku wa Jumapili wa Julai 9,2017 ndani ya Mambo Club

Bendi ya mukizi kutoka Zanzibar inayopiga muzuki wa zamani ikitoa burudani

Share:

Leave a reply