French Montana atoa msaada wa Dola 100,000 Uganda

481
0
Share:

Mwanamuziki French Montana mwenye uraia wa Marekani lakini akiwa na asili ya Morocco ametoa msaada wa Dola 100,000 (Tsh. 223 milioni) kwa ajili ya kusaidia kuboresha huduma za kijamii nchini humo.

Msaada huo French ameutoa kwa Taasisi ya Mama Hope lakini pia ameanzisha kampeni mpya inayojulikana kama Unforgettable Dance Challenge ambayo ina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia jamii kuondokana na umaskini.

Baadhi ya shughuli ambazo pesa hizo zitatumika kufanya ni kujenga kituo cha afya (Suubi Health Center) na benki ya kuhiadhia damu.

Akizungumzia msaada huo, French Montana alisema, “Muda mwingine Mungu anakupa uwezo wa kuwa sehemu fulani ili uwasaidie na watu wengine. Nataka niwape kile nilichonacho na kuwasaidia haraka iwezekanavyo.”

French Montana kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Unforgettable ambacho video yake imerekodiwa nchini Uganda akiwa na kikundi cha vijana cha Ghetto Kids.

Share:

Leave a reply