Fuvu la kichwa lazua taharuki makaburini Sengerema

331
0
Share:

Wananchi wa kata ya Nyampulukano, wilayani Sengerema Mkoa Mwanza wanaiomba serikali ifanye jitihada za haraka kutenga maeneo mengine ya maziko kutona na maeneo ya sasa  kujaa na kuleta adha kwa wananchi wanakwenda kusitili mwenzao.

Kauli hiyo ya wananchi imekuja baada ya wananchi wa kata ya nyampulukano walipokuwa wakichimba kaburi  katika makaburi ya waisilamu yaliyoko kitongoji cha uwanja wandege katika mji wa sengerema baada ya kukutana na fuvu katika maeneo hayo yanayosababishwa na maeneo hayo kujaa.

Walisema kuwa katika maisha ya kawaida ya mwanadamu anapofari kiriki ni haki yake kuzikwa na eneo alilozikwa hatakiwi kubuguziwa lakini hali ya kubuguziwa imetokea mjini sengeremakutokana na maeneo a maziko kujaa na wananchi kuutupia lawama uongozi wa halimashauri ya Sengerema kutokutilia maanani swala la kutenga maeneo ya maziko huku wakijua maeneo mengine  hayana nafasi ya kuzika tena watu waliopoteza uhai.

Baadhi ya Wananchi waliokuwa wanachimba kaburi na kukutana na fuvu hilo Lenson Masatu na Kibisa Myoba walisema kuwa  nijambo la kushangaza kwa serikali kutokuona swala hili la kutenga maeneo mengine ndiyo sababu ya kurudia kuzika mtu mwinge juu ya mwingine kitendo ambacho siyo cha kiungwana na kinadhalilisha utu wa mwanadamu na kuwaomba walitazame swala hili kwajicho la huruma  kwa wanandamu

Diwani wa kata ya Nyampulukano Emanuel  Munwazi [Chadema] aliyekuwa amehudhuria kuchimbaji wa kaburi hiyo na kukutana na fuvu hilo alisema kuwa amekwisha wasilisha hoja hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani la halimashauri hiyo lililopita  juu ya maeno hayo  ya maziko kujaa  na maazimio kutotewa lakini cha kushangaza  hadi sasa serikali haijaona umuhimu wa swala hilo ambapo linaweza kusababisha kuleta maafa kwa watu wakiono kuwa mtu wao alikuwa amezikwa kasha kufukuliwa kuzikwa mwingine.

‘’Ni jambo la kushangaza na kusikitisha juu ya swala hili kuona serikali haitilii maanani swala hili huku wawakilishi wa serikali wapo mkurugenzi yupo, mkuu wa wilaya hupo wameka kimya huku swala kutenga maeneo liko chini ya uwezo wao wanataka mauwaji  yatokee ndipo watenge maeneo hili ni aibu kwa serikali,” alisema Munwazi.

Kaburi hilo lilikuwa ni la kumzika Said Bihemo  aliyfaliki dunia  wilayani sengerema walimuzika na kishwa fuvu hilo kuliludisha ndani ya kaburi hilo walichimba  baada ya kuzika said kitendo ambacho kilizua vilio na huzuni kutawala katika makaburi hayo.

Mkurugenzi wa halimashauri ya Sengerema, Chalya Julias alisema kuwa changamato ya maeneo la maziko kujamaa yako kila kona ya sengerema hivyo  halimashauri yake iko mbioni kutafuta maeneo ya maziko sehemu nyingine kutokana na maziko hayo kujaa na kuwaomba wananchi wawe na subila juu ya swala hilo litatekelezwa. na wakumbuke kuwa kupata maeneo nilazima watu wenyemaeneo hayo walipwe.

Mwenyekiti wa halimashauri ya Sengrema, Yanga Makaga alisema kuwa anaona huruma kuona watu walipoteza uhani wakifukuliwa na kuzikwa mwingine nakuahidi  kulishugulikia swala hilo mapema   la kutenga maeno mapya ya maziko. hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu.

Na Daniel Makaka

Share:

Leave a reply