Gareth Bale na Cesc Fabregas waitolea nje Manchester United

734
0
Share:

Kumbe kama mambo yangekwenda kama jinsi yalivyopangwa yawezekana kabisa kwa sasa Gareth Bale, Cesc Fabregas na Toni Kroos wangekuwa wakicheza soka katika klabu ya Manchester United lakini kutokana na dili zingine ambazo walikuwa wakizipata wakaipotezea Man United.

Hilo limejulikana baada ya kocha wa zamani wa an United, David Moyes kuzungumza kuhusu maisha yake ya soka wakati akifundisha timu hiyo na kusema kuwa mpango wake mkubwa ulikuwa ni kuiwezesha Man United kuzidi kuwa na mafanikio hivyo alihitaji kikosi bora ambapo alihitaji kuwa na wachezaji kama Bale, Farbegas na Kroos lakini ilishindikana.

“Mara ya kwanza nilipofika, Gareth Bale alikuwa ni mtu wa kwanza kumhitaji. Nilihitaji Bale awe mchezaji wa Manchester United, nilipambana mpaka dakika ya mwisho na tulitoa ofa kubwa kuliko Real Madrid lakini yeye na akili yake akachagua kwenda Real Madrid lakini alikuwa mchezaji ambaye nilimhitaji sana,

“Mwingine alikuwa ni Cesc Fabregas ambaye tuliamini tungepata mwafaka mpaka dakika ya mwisho. Nakumbuka, wakati nakutana na Sir Alex kwa mara ya kwanza aliniambia pia kuna uwezekano wa kumrejesha Ronaldo,” alisema Moyes na kuongeza.

“Toni Kroos alikubali kuja katika majira ya joto. Nilikuwa nimekubaliana na Toni mwenyewe na wakala wake na hiyo ndiyo hatua ambayo tulikuwa tumefikia, tulikuwa na kikosi ambacho kimetoka kushinda mataji hivyo tulihitaji kwenda mbele zaidi.”

Share:

Leave a reply