Gareth Barry avunja rekodi ya Ryan Giggs, Arsenal yampa zawadi

224
0
Share:

Mchezaji wa klabu ya West Brom Albion, Gareth Barry amevunja rekodi iliyowekwa na mkongwe wa Manchester United, Ryan Giggs ya kucheza michezo mingi ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Barry anevunja rekodi hiyo na kuweka rekodi yake mpya ya kucheza michezo 633 katika mchezo wa wa Arsenal na West Brom uliopigwa katika dimba la Emirates na Arsenal na kuibuka na ushindi wa goli 2-0 akimwacha Giggs ambaye amecheza michezo 632.

Akizungumzia rekodi hio, Barry alisema,”Ni wakati mzuri sana kwangu na ninajivunia kufikia mafanikio hayo lakini kama jambo lingine lolote nitaendelea kuongeza juhudi ili kushinda kila mchezo.”

Kwa upande wa Giggs amempongeza Barry kwa kuvunja rekodi aliyokuwa ameiweka na kumtakia mafanikio mema, “Ni mafanikio makubwa, najua wewe ni mchezaji wa kiwango kikubwa na kucheza michezo mingi katika kiwango kikubwa ni mafanio makubwa, hongera sana natumai kuna michezo mingi zaidi inakuja.”

Baada ya kuweka rekodi hiyo katika mchezo wa Arsenal, kocha wa Arsene Wenger alimpa zawadi ya jezi ambayo ina namba ya michezo 633 ambayo Barry amecheza.

Orodha ya wachezaji ambao wamecheza michezo mingi ya Ligi Kuu ya Uingereza;

Gareth Barry – 633

Ryan Giggs – 632

Frank Lampard – 609

David James – 572

Gary Speed – 535

Emile Heskey – 516

Mark Schwarzer – 514

Jamie Carragher – 508

Phil Neville – 505

Rio Ferdinand – 504

Steven Gerrard – 504

Share:

Leave a reply