Guardian ya pili kwa usalama wa habari za mtandaoni

417
0
Share:

Orodha iliyotengenezwa na Freedom of the Press Foundation, Shirika lilsilotengeneza faida la Marekani limesema kwamba Guardian ni ya pili kwa namna ambavyo inavyowezesha usalama wa habari wanazozitoa katika tovuti.

Orodha hiyo imetengenezwa kwa kuangalia namna ambavyo saiti hizo zinasapoti teknolojia ambapo ufaragha na usalama wa wanaotembelea eneo hilo wapo salama kwa kuwa wanatumia HTTPS, protoko ya tovuti ambayo inaruhusu maunganisho kwa mfumo wa encrypted.

Orodha hiyo inaongozwa  na twebu saiti ya Marekani ya  The Intercept, ambayo imeundwa na mwanzilishi wa eBay, Pierre Omidyar.

Wengine waliokwenda sawa na Guardian, ni TechCrunch na ProPublica.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia The Freedom of the Press Foundation imewataka wachapishaji kulinda haki za watu wanaowatembelea (wasomaji).

Share:

Leave a reply