Habari njema kwa Watanzania, Samatta asajiliwa na klabu ya Ubelgiji, stori kamili ipo hapa (picha)

283
0
Share:

 

Mbwana Samatta akiwa na jezi ya klabu yake mpya

Sama goal

Mbwana Samatta akitambulishwa katika mkutano na waandishi wa habari

Na Rabi Hume, Modewjiblog

Licha ya kung’aa katinga anga la burudani nyota ya Tanzania inazidi kukua siku baada ya siku ambapo mwanzoni kwa mwaka 2016, Tanzania ilifanikiwa kutoa mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani baada ya Mbwana Samatta kutwaa tuzo hiyo.

Nyota hiyo imezidi kung’aa baada ya mchezaji huyo, Samatta kufanikiwa kujiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne ambao utamwezesha Samatta kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2019.

Akizungumza katika mkutano wa kutambulishwa kwenye klabu hiyo Samatta alieleza kuwa wazo la kujiunga na klabu hiyo baada ya kukutana na mmoja wa viongozi wa klabu ya Genk wakati akiwa na klabu yake ya zamani ya TP Mazembe ilipokuwa katika Mashindano ya Klabu Bingwa Dunia.

Samatta alisema kuwa anatambua Genk kuwa klabu kuwa na ambayo imewatoa wachezaji wengi wakubwa na kuwepo kwake klabuni hapo atatumia uwezo wake wote kuisaidia klabu hiyo kushinda michezo yao la ligi na kufanikiwa kutwaa makombe.

 Aidha Samatta amechukua namba 77 ya klabu hiyo akisema kuwa ameamua kuchagua namba hiyo kutokana na mapenzi yake na jezi namba saba na kutokana na namba hiyo kuvaliwa na mtu mwingine amechukua namba hiyo kutokana na kuwa na namba saba mbili ambazo anaamini hajakosa kitu.

Mbwana Samatta

Samatta 2

Samatta

Share:

Leave a reply