Hali ya MC Pilipili aliyepata ajali Shinyanga yaimalika,alazwa Bugando

357
0
Share:

Daktari wa Hospitali ya Bugando Dk. Hans Cloud ambaye yupo katika kitengo cha magonjwa ya dharura, amebainisha kuwa, hali ya  Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Emmanuel Mathias (Mc Pilipili) aliyelazwa Hospitalini hapo inaendelea kuimalika baada ya kuendelea na matibabu ktokea alipoletwa hapo.

Dk. Cloud anasema hadi sasa anaendelea vizuri na bado anaendelea na matibabu zaidi chini ya uangalizi wa madaktari bingwa Hospitalini hapo.

“Tulimpokea jana kitengo cha dharura. Awali alikuwa na maumivu sehemu za mgongo pamoja na tatizo tumboni na kukosa ufahamu kiasi hivyo timu nzima ya Madaktari tuliweza kufanya vipimo mbalimbali vya matibabu na hadi sasa anaendelea vizuri” alieleza Dk. Cloud

MC Pilipili amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya gari Mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule amesema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa kumi alasiri katika Kijiji cha Mwanishoni, Kata ya Bubiki wilayani Kishapu katika barabara ya Mwanza-Shinyanga.

Amesema ajali hiyo ilihusisha gari binafsi lenye nambari T.362 BAE Toyota Prado iliyokuwa na abiria watatu ikiendeshwa na dereva Said Hassan (28) mkazi wa Dar es salaam, ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam.

Chanzo: BMG

Sikiliza hapa kutoka Hospitali ya Bugando

MC PILIPILI

Share:

Leave a reply