HALOTEL YATOA BURUDANI NA ELIMU VYUONI KUPITIA ‘HALOTEL FRESHERS’

202
0
Share:

Kampuni ya simu Halotel ikiwa ni mtandao unaopendwa zaidi na wanafunzi wa vyuo yawaletea burudani wanafunzi wa vyuo vikuu  katika chuo cha Dar es salaam Kupitia tamasha lake la Halotel Freshers bonanza lililofanyika katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wanafunzi.

Tamasha hilo la burudani lilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa bongo fleva  Dully Sykes and Stamina, michezo mbalimbali pia lilitawaliwa na watu mashuhuri ambao walikuja kuongea na wanafunzi kuhusiana na jinsi ya kujitambua  kutatua changamoto mbalimbali  pindi wanapokuwa shule lakini pia jinsi ya kujiandaa baada ya kuhitimu masomo yao na elimu ya kujiajiri.

Bonanza hilo lililoanza majira ya asubuhi ambapo wanafunzi waliweza kushirikikatika michezo mbali mbali kama vile Netiboli, soka na kukimbia na mingineyo, ambapo shule mbalimbali zilizopo chuoni hapo ziliweza kuchuana ikiwa ni hali ya kuendeleza utamaduni kwa wanafunzi kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao.

Akizungumzia kuhusiana na tamasha hilo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Halotel, Bwana Mhina Semwenda alisema tamasha hilo lina lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Halotel na wanafunzi wa vyuo vikuu.toka mtandao wetu umeanza hapa nchini tumejikita katika kuhakikisha tunaboresha huduma mawasiliano nchini, lakini kwa upekee kabisa tumekuwa tunawapa wanafunzi huduma za kipekee ,bora na kwa gharama  nafuu zaidi kwasababu tunajua uitaji mkubwa  wa mawasiliano na internet kwa wanafunzi katika maisha yao ya kujifunza alisema bwana Semwenda.

Kwa upande wa watu mashughuli walio shiriki katika katika Halotel freshers Bonanza ambao na wao walipitia katika chuo hicho, ikiwamo Mwandishi Mkongwe wa vitabu hapa nchini Bwana Constantine Magavila ambapo aliongea na wanafunzi juu ya ujasiria mali na uthubutu hata wakiwa katika mazingira ya shule. Pia aliwapa neno la umuhimu wa kujitambua na kuwa tayari kujifunza, kuwa na uwezo wa kushawishi na kujiamini.

Kwa upande wa burudani Stamina na Dully Sykes walipopanda jukwaani walitumia takribani saa 2 kuzikonga nyoyo za mashabiki wao hao ambapo waliimba na kucheza nao pia hasa akionesha umahiri wao wa kucheza dansi.

Kwa upande wake waziri wa michezo wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, bwana David Mabina aliishukuru kampuni ya Halotel kwa kufanikisha tamasha hilo.Tunawashukuru sana Halotel kwa kufanikisha tamasha hili, na kama unavyoona wanafunzi wamepata kujifunza na kuburudika lakini pia kubadilishana mawazoâ alisema Mabina.

Wanafunzi wa vyuo wakipata burudani katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Msanii Mkongwe nchini Tanzania wa nyimbo za kizazi kipya Duly Skyes, akitoa burudani kwa wanafunzi katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Stamina, akitoa burudani kwa wanafunzi katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi hao wakishiriki mchezo wa kufukuza kuku katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi hao wa vyuo wakiendelea na mchezo wa mpira wa miguu katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam wakicheza Valley ball katika Tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Nguyen Van Son (Wa tatu Kushoto) akikabidhi zawadi ya kombe na Mpira kwa washindi wa kwanza ( Freshers) wa mchezo wa mpira wa mguu katika tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel liitwalo Halotel Freshers Bonanza kwaajiliya wanafunzi wa chuo lililofanyika jana katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply