Hans Poppe afuta uamuzi wa kujiondoa kwenye uongozi wa Simba SC

425
0
Share:

Ikiwa imepita siku moja tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe atangaze kujiuzulu nafasi hiyo, leo jumatatu ya mei, 15 amefuta uamuzi huo na kurejea katika nafasi yake.

Taarifa ya Hanspoppe kurejea katika nafasi hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Manara ameandika,”Rasmi Hanspope arejea kundini,,afuta uamuzi wake wa kujiuzulu,, na ndio maana fans wetu nawaomba mtulie,,hakuna kitakachoharibika ,ni upepo mbaya ulipita na sasa umetulia,,Karibu tena kamanda Pope.”

Share:

Leave a reply