Harusi Trade Fair kufanyika nchini mwezi Mei

404
0
Share:

Zaidi ya wafanyabiashara 30 watashiriki kutoa huduma na kuuza bidhaa za maharusi katika maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 12 hadi 13,2017 katika hoteli ya Golden Tulip Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Meneja Biashara wa Maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya 360 Degree, Hamis Omary wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, amesema maonyesho hayo yatarahisisha maandalizi ya harusi kwa kupata bidhaa bora za harusi.

“Maonesho haya ni ya kipekee kwa Afrika Mashariki yanayofanyika mara moja kwa mwaka, yatakua ya kuvutia, kuburudisha pamoja na nyakati rahisi kwa maharusi kuandaa vitu vya harusi. Kutakua na mitindo mipya kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi,” amesema.

Mratibu wa Maonesho hayo, Naomi Godwin amesema maonesho hayo hayatakua na kiingilio na kuwataka watu kuhudhuria kwa wingi kwenye maonesho hayo yatakatosheheni bidhaa bora za harusi.

“Na kama ilivyoa ada kuwa mwanzo wa msimu wa harusi kwa watanzania umeanza na maonyesho haya si ya kukosa ili watu waweze kuona ubunifu wa vipaji vya watanzania waliopo kwenye sekta ya harusi na kuzifanya harusi zao kuwa ukumbusho wa pekee,” amesema.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply