Hatuwezi kufanya mabadiliko kwa mashinikizo kutoka nje-Tanzania

298
0
Share:

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,  amewaeleza wakuu wa UNICEF kwamba, mabadiliko ya kweli yanayolenga kuboresha hali bora ya maisha ya makundi yote ya jamii, wakiwamo watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali hayawezi kufanyika kwa mashinikizo kutoka nje bali yatafanyika kwa ushiriano na ubia wa dhati baina ya Serikali, Wadau wa Maendeleo na Wananchi wenyewe.

Balozi Manongi ameyasema hayo wakati wa kuchangia majadiliano ya Bodi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto ( UNICEF) katika mkutano huo uliofanyika mapema 2 Februari.

Vile vile Balozi Manongi akasisitiza kwamba UNICEF inapashwa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia bajeti iliyojipangia badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani, hususani Asasi zisizo za kiserikali kwa kile alichosema, mara nyingi Asasi hizo hutoa misaada yao kwa malengo ya kushinikiza ajenda zao na maslahi binafsi.


Mkutano huo pia ulipokea na kupitisha mpango kazi wa utekelezaji wa miradi ya UNICEF pamoja na rasimu ya Ripoti ya Tanzania ambayo imeainisha masuala mbalimbali pamoja na miradi ya maendeleo inayorajiwa kutekelezwa na UNICEF kwa Tanzania.

IMG_3987---CopyMwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akichangia mada katika mkutano huo wa UNICEF. Aliyeketi na Balozi ni Afisa wa Uwakilishi Bi.Ellen Maduhu

IMG_3994---CopyMeza kuu ya Wakurugenzi na Watendaji wa UNICEF wakati wa mkutano wa Bodi hiyo uliofanyika siku ya jumanne na kuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi hawapo picha pamoja na wajumbe wengine waalikwa. Tanzania ilialikwa katika mkutano huo kama msikilizaji.

Share:

Leave a reply