Heart Marathon yafana Dar es Salaam

330
0
Share:

Picha za matukio ya Heart Marathon iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  ambapo ilihusisha mbio za urefu wa 21Km, 10Km, 5Km, mita 700 kwa ajili ya watoto, Baiskeli Kilomita 21 na Baiskeli walemavu.

HM3b

Washiriki wa mbio za Heart Marathon kwa waendesha Baiskeli wakiwa katika mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.

HM3c

Watoto wakiwa katika mashindano ya Heart Marathon  mbio za urefu Mita 700 jana jijini Dar es Salaam.

HM3a

Wanariadha washiriki wa Heart Marathon wakichuana katika mbio za urefu wa kilomita 21 jana jijini Dar es Salaam.

HM4a

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanaume mbio za Kilomita 21  Bw. Dickson Marwa wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

HM4b

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanawake mbio za Kilomita 21  Bibi. Failuna Abdi wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

HM5

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akikabidhi Tuzo kwa mdhamini mkuu wa mbio za Heart Marathon, Taasisi ya Tindwa Medical and Health Services wakati wa ufungaji wa mbio za hizo jana jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilikuwa na kauli mbiu ya “Kuwa huru katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza”.

HM1

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na wadau wa riadha wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Half Marathon zilizofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kongamano la Afya Tanzania na Mratibu wa mbio hizo Dkt. Omary Chillo.

HM2

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chakao Khalfan akizungumza na waandishi wa Habarai mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jana jijini Dar es Salaam. Heart Marathon hii imejumuisha mbio za urefu wa 21Km, 10Km, 5Km, mita 700 kwa ajili ya watoto, Baiskeli Kilomita 21 na Baiskeli walemavu.(Picha na: Frank Shija, WHUSM).

Share:

Leave a reply