Hiki ndicho alichokisema Barack Obama na Angela Markel baada ya taarifa ya David Cameron kujiuzulu

248
0
Share:

Baada ya wananchi wa Uingereza kupiga kura za kujitoa Umoja wa Ulaya na kura za kujitoa kuwa asilimia 51.9 ambazo ni sawa na wapiga kura 17,410,742 na waliotaka kuibakisha Uingereza wakiwa ni asilimia 48.1 sawa na wapiga kura 16,141,241 hivyo waliotaka ijitoe kuwa wengi hali iliyofanya Waziri Mkuu wa taifa hilo, David Cameron kutangaza kujiuzulu viongozi mbalimbali duniani wametoa maoni yao.

Hatua ya Cameron kutangaza kujiuzulu na kusema kuwa ataondoka madarakani mwezi Oktoba imekuja baada ya kushindwa kuwashawishi Waingereza kusalia katika Umoja wa Ulaya (EU) huku akisisitiza kuwa hakuona umuhimu wa Uingereza kujitoa EU kwani walikuwa na nafasi nzuri.

Kansela wa Ujerumani, Angela Markel amesema uamuzi wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya limekuwa jambo la kushtusha kwao na litawaachia majuto makubwa.

Kwa upande wa Rais wa Marekani, Barack Obama amesema pamoja na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya lakini hilo haliwezi kuathiri uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo.

Nae Rais wa Umoja wa Ulaya (EU), Jean-Claude Juncker anaamini mazungumzo ya Uingereza kuondoka EU yataanza haraka iwezekanavyo japo watakuwa na machungu ya kuondoka Uingereza wakati wakifanya mazungumzo hayo.

Share:

Leave a reply