Hisa za kampuni ya ACACIA Mining katika soko la DSE zapanda kwa 15%

332
0
Share:

Bei ya hisa za kampuni ya Acacia Mining katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imepanda kwa asilimia 15 kutoka Sh. 4,980 hadi 5,710, wakati bei ya hisa za Kampuni ya Vodacom ikipanda kwa 10% na NMG kwa 1.27.

Hayo yameelezwa leo na Meneja Masoko Mwandamizi DSE, Marry Kinabo wakati akitoa taarifa ya kila wiki ya soko hilo. Na kusema kuwa, kupanda bei za hisa za kampuni hizo kumepelekea ukubwa wa mtaji wa Kampuni zilizo orodheshwa katika DSE kongezeka kwa Sh. Bil. 431 kutoka Tril. 20.3, na ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Mil. 187 kutoka Tril. 9.7 hadi Tril. 9.9, wiki iliyopita hadi Tril. 20.8 wiki iliyoishia Oktoba 6, 2017. 

Hata hivyo, Kinabo amesema thamani ya mauzo ya hisa katika soko hilo imepungua kutoka  Bil.3 hadi kufikia Bil. 1.5, vilevile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa laki 8 katika kipindi cha wiki iliyoishia septemba 29, 2017 hadi hisa laki 6 wiki iliyoishia oktoba 6 mwaka huu.   

Kwa upande wa viashiria, amesema kiashiria cha kampuni zilizo orodheswa DSE (DSEI) kimepanda kwa pointi 45 kutoka 2,116 hadi 2162 baada ya kupanda kwa bei za hisa za kampuni ya Acacia Mining, Vodacom Tanzania PLC. Kiashiria cha kampuni za ndani kimepanda kutoka pointi 3,742 hadi 3,814, na cha sekta ya viwanda kimepanda kutoka 5,143 hadi 5,161. 

Pia amesema kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimepanda kutoka 4,633 hadi 5,034, wakati kiashiria cha huduma za kibenki na kifedha kikibaki kwenye wastani wa pointi 2,515.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply