Hizi kweli akili za usiku, Suarez na Neymar kuwania burger

283
0
Share:

Kuelekea kwa mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu nafasi ya kucheza kombe la mataifa kwa nchi za Amerika ya Kusini baina ya Uruguay na Brazil, mastaa wa mataifa hayo wawili, Luis Suarez na Neymar wametoa kali ya kuwania burger.

Akizungumza na gazeti la El Mundo Deportivo la Hispania, Suarez alisema amekubaliana na mchezaji mwenzake Neymar kuwa atakayefungwa katika mchezo huo ndiyo atakayemnunulia mwenzake burger.

“Nime’bet’ burger na Neymar, yoyote atakayepoteza atatakiwa kumlipa mwenzake,

“Neymar ni rafiki yangu wa karibu, huwa tunataniana tukiwa Barca. Juu ya yote sisi tunacheza timu moja na ninaamini ushindi wowote tutafurahia na kupoteza pia tutapokea matokeo,” alisema Suarez.

Mchezo huo wa Uruguay na Brazil utakuwa mchezo wa kwanza kwa Suarez kuichezea timu yake ya taifa, La Celente tangu Juni 24, 2014 baada ya kufungiwa kuchezea timu ya taifa michezo tisa kwa kumg’ata meno beki wa Italia, Giorgio Chiellini.

Share:

Leave a reply