Huawei yazindua Programu ya ‘Seeds for the Future’ nchini

198
0
Share:

Kampuni ya Huawei inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulimwenguni, leo imezindua programu ya elimu inayoitwa Seeds for the Future hapa nchini Tanzania.

Programu ya ‘Seeds for the Future’ inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa hapa nchini kutoka vyuo vikuu kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China.

Mradi huo umelenga kuwa kusaidia kile kinachofundishwa shuleni kukidhi mahitaji halisi ya soko la ajira kwa vijana hapa nchini ikiwa ni pamoja na kupanua uelewa wa TEHAMA na kuhamasisha ushiriki katika sekta hii ili kuendana na  jamii ya sasa teknolojia ya habari na mawasilino.

Akizunguma wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliochaguliwa kusoma China, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Bruce Zhang alisema ni wazi kwamba wanafunzi hawa watapewa kipaumbele kwenye fursa za kujifunza kupitia kujumuika na wafanyakazi wa Huawei na kutembelea maabara ya kampuni hiyo ambako wataweza kuona na kufanya majaribio ya teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano.

Alisema vijana hao watapa ujuzi wa kisasa unaowawezesha kushindana katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, huku wakijufunza kukabiliana na ushindani katika soko la ajira.

 “Uzinduzi wa mpango huu inathibitisha kuwa tutaendelea kusaidia sekta ya TEHAMA hapa nchini,” alisema mkurugenzi huyo.

“Kupitia ushirikiano huu na Huawei, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ninaamini wanafunzi hawa watakuwa na fursa ya kipekee kufanya kazi na kusoma makao makuu ya Huawei, huku wakijifunza utamaduni wa China na kutembelea maeneo muhimu ya vivutio vya utalii,” alisema Bruce

Alisema, mradi huu unafanyika kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni ambako Kampuni ya Huawei inafanya shughuli zake na hapa nchini mpango umeshaandaliwa kwa wanafunzi 10 ambao watashiriki programu hii China na watasafiri Mei, 20 mpaka Juni, 3 ambapo watashiriki mafunzo hayo muhimu.

Alisema, ‘Seeds for the Future’ ni jambo linalodhihirisha kwamba Huawei imeweka mkazo katika maendeleo ya elimu ya TEHAMA vyuo vikuu kama jinsi ilivyojidhihirisha wakati wa kuzindua mradi huu wa elimu”

Naye Mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Simon Msanjila alisema kuanzishwa kwa programu hii ni ushahidi kwamba Kampuni ya Huawei imedhamiria kusaidia maendeleo ya TEHAMA katika vyuo vikuu nchini pamoja na kuifanya Tanzania kung’ara katika teknolojia ya habari na mawasiliano.

 “Hii itawawezesha wanafunzi wetu kujifunza kwa kuelewa na kuwaandaa kuwa wafanyakazi mahiri kwenye masuala ya IT na sekta ya mawasilino,” alisema Profesa Msanjila.

Naibu Katibu huyo wa Elimu aliongeza kwamba; “Programu ya Seeds for the Future itawasaidia wanafunzi kutoka vyuo hivyo viwili kujifunza mambo mengi ili kuendana na mahitaji ya soko la dunia kwenye TEHAMA.

4 (2)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mhe. Abdullah Mzee akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya elimu ya Huawei ”Seeds for the future” ambayo inatoa nafasi 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China ambapo watajizolea ujuzi. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma.

8

Wageni wa Meza kuu na baadhi ya wafanyakazi wa Huawei wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi 10 wa vyuo vikuu nchini ambao kupitia programu ya “Seeds for the Future” inayodhaminiwa na Huawei walichaguliwa kwenda China kujifunza na kufanya kazi na kampuni hiyo yenye makao makuu yake Shenzhen, China. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma.

9

Mkurugenzi wa Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi 10 wa vyuo vikuu nchini mara baada ya uzinduzi rasmi wa programu ya elimu ya Seeds for the future ambayo inadhamini wanafunzi 10 wa vyuo vikuu hapa nchini kila mwaka kwenda China kujifunza na kufanya kazi na kampuni hiyo yenye makao makuu yake Shenzhen. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma.(Kulia) ni Mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Prof. Simon Msanjila na (katikati) ni mwakilishi wa balozi wa China nchini.

10 (1)

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania Samson Majwala (katikati) akifafanua jambo kwa wageni wa meza kuu kuhusiana na bidhaa za Huawei wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa programu ya Huawei ya “Seeds for the Future” ambayo inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei iliyopo Shenzhen, China. Programu hiyo ambayo itadumu kwa muda wa miaka 10 ilizinduliwa rasmi mjini Dodoma.

Share:

Leave a reply