Huduma ya ‘Total wash’ yazinduliwa Dar

138
0
Share:

Kampuni ya mafuta ya Total imezindua huduma mpya na maalumu ya kuosha magari ijulikanayo kama “Total Wash” ambayo kwa sasa inapatikana katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mauzo wa Total Tanzania, Nikesh Mehta alisema huduma hiyo mpya ina lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwani wateja wataoshewa magari yao kwa haraka zaidi kwa kupitia utaalamu wa ‘jet wash.

“Tunalo lengo pia la kuhakikisha kuwa huduma zote zinapatikana katika kituo kimoja hasa kwa wateja wa Total ambao hawana muda mrefu wa kusubiri tutahakikisha wanapata huduma iliyo bora baada ya kujaza mafuta na kupata huduma nyingine za kiufundi tunazotoa,” alisema.

Alisema huduma hiyo imepokewa vizuri na wateja katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access.

“Kuna sehemu nyingi za kuosha magari lakini huduma hii ni ya kipekee kutokana na utaalamu na teknolojia inayotumika ambayo itahakikisha wateja wa Total wanapata huduma iliyo bora na ya viwango vya juu,” alisema na kuwataka wateja wengi zaidi wajaribu huduma hiyo.

Alisema kwa wateja wanaohitaji kutumia huduma hiyo, wanatakiwa kununua sarafu maalumu (token) katika maduka ya Total (Café Bonjour) yanayopatikana katika vituo vyao na kila sarafu itakuwa na kipimo cha muda kulingana na huduma inayotolewa..

Bw. Mehta alisema wana mpango wa kuanzisha huduma hiyo katika vituo zaidi nchini katika siku za hivi karibuni.

Total ina vituo 90 nchi nzima na inajivunia kwa kuuza mafuta na vilainishi vyenye ubora wa hali ya juu kama vile Total Quartz, Total Rubia na Special 4T lakini pia inajivunia kutoa huduma zinazoaminika na kukubalika kote.

Share:

Leave a reply