HUDUMA ZA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WA KEREGE 27 NOVEMBA

341
0
Share:

Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imeandaa kambi ya matibabu ya bure itakayofanyika eneo la Kerege wilayani Bagamoyo. Huduma hizo za matibabu zitatolewa siku ya Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.

Timu ya wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali, wanafunzi wa udaktari, wanachama wa Rotary na wafanyakazi wa kujitolea kutoka sekta mbalimbali watashiriki katika kambi hiyo ya matibabu.

Vipimo na matibabu yatatolewa kwa magonjwa kama malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho, meno na kansa ya kizazi kwa akina mama. Miwani zitatolewa kwa watu watakaokutwa na matatizo ya macho. Huduma za ushauri kwa wajawazito zitatolewa na wajawazito pia watapatiwa vifaa vya kujifungulia bure.

Wakazi wa Kerege na maeneo ya jirani wanaombwa kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo ya matibabu ya bure haswa akina mama na watoto.

Akizungumza kuhusu mradi huu, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema, “Tuna furaha kuandaa kambi hii kwa mara nyingine tena kwa wakazi wa Kerege ambapo lengo letu ni kuwasaidia watu ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu. Tunawashukuru wadhamini na watu wote wanaojitolea katika mradi huu na tunakaribisha watu kuhudhuria na kusaidia kwa namna yoyote ile katika kambi hii ya matibabu.”

Usajili wa matibabu utaanza mapema asubuhi na watu wapatao 1,200 wanatarajiwa kupata huduma za matibabu kulingana na mwenendo wa idadi ya watu ambao huwa wanajitokeza kila mwaka kambi hiyo inapofanyika. Wakazi wa Kerege wanashauriwa kufika mapema ili kuweza kupata huduma.

Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na inaandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.

 Kambi ya Matibabu

Kambi ya kwanza ya Matibabu kuandaliwa na Klabu Ya Rotary ya Oyster Bay ilifanyika Chanika mwaka  2011 na zaidi ya watu 600 walipimwa malaria, UKIMWI, kisukari, Masikio, Pua na Koo, Macho na magonjwa mengine sugu.

Dawa pamoja na miwani zilitolewa bure kwa watu waliokutwa na matatizo. Mwaka 2012 watu zaidi ya 700 walipatiwa matibabu, sawa na mwaka 2013 na 2014. Mwaka 2015 idadi ya watu waliopata huduma ilipanda hadi kufikia zaidi ya watu 1,200. Mwaka huu pia idadi hiyo ya watu 1,200 inatarajiwa kupata matibabu.

dsc_0318

Rais wa rotary Klabu ya Oster Bay akielezea lengo la matibabu haya kwa wakazi wa kerege bagamoyo.

Kuhusu Rotary

Rotary ni mtandao wa watu zaidi ya milioni 1.2 duniani kote ambao hukutana ili kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu kwenye jamii, katika jamii na duniani kote. Kutokana na mchanganyiko wa wanachama wenye ujuzi, utamadani , na wanaotoka kwenye nchi tofauti, Rotary ina mtazamo wa kipekee katika matatizo yanayoikabili jamii. Rotary inaundwa na watu wenye moyo wa dhati wa kusaidia jamii na wenye nia madhubuti ya kutimiza malengo waliyojiwekea.

Kazi zote nzuri zinazofanywa na Rotary ni kupitia wanachama wake ambao hufanya kazi bila kuchoka katika klabu zao ili kutatua baadhi ya matatizo makubwa katika jamii zetu.

Rotary imebainisha maeneo makuu ya kufanyia kazi katika jamii. Wakati huo huo tunatambua kuwa kila jamii ina mahitaji na matatizo ya kipekee ambayo yanaweza yasiwe sawa na ya jamii nyingine.  Kupitia mtandao wa Rotary wa rasilimali na  washirika mbalimbali, klabu za Rotary duniani kote zina vipaumbele katika kukuza amani, vita dhidi ya magonjwa, kutoa maji safi na salama, kuokoa wakina mama na watoto, kusaidia elimu pamoja na kukuza uchumi katika jamii

ROTARY CLUB

Mkuu wa kitengo cha sheria Bw. Ives Mlawi kutoka DTB akiongea na wanahabari kuhusu DTB kudhamini gharama za matibabu 

Share:

Leave a reply