Idadi ya watu waliokufa katika ajali ya ndege Colombia yatajwa

1495
0
Share:

Usiku wa kuamkia Jumanne ya Novemba, 29 unaingia katika historia ya nchi ya Brazil na Colombia baada ya kutokea ajali ya ndege ambayo ilikuwa imebeba abiria na wachezaji wa klabu ya Chapecoense ya Brazil na kuanguka nchini Colombia kabla ya kutua katika uwanja wa ndege.

Baada ya kukamilika kwa utafiti wa awali umeonyesha kuwa ndege hiyo ilikuwa na watu 81 wakiwepo wachezaji, wahudumu wa ndege na waandishi wa habari 21 na waliopoteza maisha ni watu 76, ambapo kati ya watu watano waliopona, watatu ni wachezaji wa Chapecoense.

Wachezaji hao wametajwa kwa majina kuwa ni Alan LucianoRuschel, Marcos Danilo Padilha na Jacson Ragnar Follmann.

“Watu sita walikutwa wakiwa wazima, lakini kwa bahati mbaya mtu mmoja amefariki. Wengine waliosalia wamepoteza maisha na hivyo jumla yao wote ni 76,” alisema Kamanda wa Polisi Medellin, Jose Geardo Acevedo.

Kwa upande wa klabu ya Chapecoense haijatoa taarifa yoyote na taarifa zinaeleza kuwa wanasubiri ripoti ya Mamlaka ya nga ya Colombia ndiyo watoe taarifa kuhusu ajali hiyo ambayo kulikuwa na wachezaji 22 wa klabu hiyo.

 

Viongozi mbalimbali wameanza kuonyesha hisia zao kuhusu tukio hilo akiwepo Rais wa Brazil, Michel Temer, golikipa wa zamani Hispania na Real Madrid, Iker Casillas pamoja na klabu ya Barcelona na Atetico Madrid.

Share:

Leave a reply