Idadi ya watu wanaokufa kwa uvutaji wa sigara kuongezeka hadi watu milioni 8 kwa mwaka

617
0
Share:

Hali ya kiafya ya watu ambao wanavuta sigara inazidi kuwa mbaya baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa ripoti ambayo inaonyesha hivi karibuni kutakuwa na watu milioni nane ambao watakuwa wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uvutaji sigara.

Vifo hivyo vimeripotiwa kuwa vitakuwa vikitokana na magonjwa ambayo watumiaji wa sigara wanakuwa nayo kutokana na matumizi ya sigara kuonekana kuongezeka ambapo kwasasa inakadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni moja kutumika kila mwaka kwa ajili ya kununua sigara.

“Vifo vya watu ambao wanatumia bidhaa ambazo zinatokana na tumbaku itapanda kutoka watu milioni sita hadi milioni nane ifikapo 2030, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zenye uchumi mdogo na wa kati,” ilisema ripoti hiyo.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa bidhaa za tumbaku ni moja ya vitu hatari kwa afya na ambavyo vimekuwa vikisababisha vifo vya watu wengi lakini bado idadi ya watumiaji wake inazidi kuongezeka kwa kasi katika maeneo mbalimbali duniani.

Share:

Leave a reply