Imani ya kidini yasababisha kufungwa kifungo cha maisha

245
0
Share:

Ule msemo wa sheria ni msumeno unakata pande zote bila kufanya upendeleo wa upande wowote umekuta mtu mmoja nchini Uingereza baada ya kujikuta akihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hati na mahakama kwa kufanya mauaji kwa ajili ya sababu za kidini.

Mtu huyo ambaye alifahamika kwa jina la Asad Shah amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumuua Tanveer Ahmed kwa sababu za kiimani kuwa inaivunjia heshima dini ya Kiislam.

Shah alifanya mauaji ya kumuua Ahmed, Machi, 24 mwaka huu wakati akiuza katika duka lake lililopo eneo la Glasgow na baadae kuacha mwili wa mtu huyo nje ya chumba ambacho anakitumia kuhifadhi bidhaa zake.

Aidha muuaji huyo alieleza kuwa alimuua Ahmed kwa sababu aliweka video katika mtandao na kujiita kuwa yeye ni nabii na baada ya kuona hivyo aliondoka kutoka eneo alilokuwepo na kwenda eneo alilopo Ahmed kisha kutekeleza mauaji hayo.

Share:

Leave a reply