India kutumia dola milioni 530 kujenga sanamu refu duniani

326
0
Share:

Mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alikwenda mji wa Mumbai kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa  sanamu la Chatrapati Shivaji, Kiongozi wa Himaya Maratha ambaye kumbukumbu  ni ya karne ya 16 na inakadiriwa kugharimu Rupia za India bilioni 36 (USD 530,000,000) sawa na (Trilion 1,151,160,000,000).

Sanamu hilo, ambalo ni kubwa kujengwa katika Bara la Asia pembezoni mwa pwani ya  Mumbai , itakuwa urefu wa mita 192 na wachambuzi wa mambo wanasema itakuwa sanafu refu kabisa katika kumbukumbu ya nchini ya India.

Kwa kulinganisha, na sanamu la Uhuru ambao ni mita 93 kwa urefu lakini sasa sanamu refu zaidi kupita yote itakuwa hilo la Shivaji kati kati ya mji wa Mumbai.

Baadhi ya sanamu zingine ndefu zaidi duniani kama vile, Laykyun Setkyar ya Buddha, ni katika mji wa  Myanmar ambao ni mita 115.8  kwa urefu .

India pia inatarajiwa kuanza kazi ya ujenzi wa sanamu ya umoja kwa ajili ya kumkumbuka Sardar Vallabhbhai Patel, naibu waziri mkuu wa kwanza wa nchini hiyo baada ya Uhuru.

Serikali inatumia Rupia 29700000000 (USD 438,000,000)juu ya mradi wa miaka minne, ambayo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa 2018.

Share:

Leave a reply