ISIL yadai kuhusika na shambulio la Barcelona lililosababisha vifo vya watu 13

750
0
Share:

Wakazi wa jiji la Barcelona nchini Hispania alhamisi ya Agosti 17 waipata taharuki baada ya kutokea shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu 13 na wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa baada ya kugongwa na gari katika eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu la Las Ramblas.

Ikiwa imepita masaa kadhaa baada ya shambulio hilo kutokea, kuundi la kigaidi la ISIL limedai kuhusika na shambulio hilo la Barcelona lililosabisha vifo kwa watu 13 na wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.

Polisi nchini Hispania wamesema wamewaua watu watano katika eneo la Cambrils wakihusishwa na tukio hilo na wakiendelea kumtafuta mtu anayetajwa kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari lililowagonga watu na kukimbia kusikojulikana.

Viongozi mbalimbali duniani akiwepo Rais wa Marekani, Donald Trump wameanza kutuma salamu za pole kwa wahanga wote wa shambulio hilo.

Serikali ya Ufaransa imethibitisha kuwa raia wake 26 ni miongoni mwa majeruhi zaidi ya 100 wa shambulio la Barcelona.

Share:

Leave a reply